Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa masharti ya kuzingatiwa wakati wanafunzi wanapoomba mikopo kwa mwaka wa fedha 2018/19 ili vigezo viweze kuzingatiwa kama ilivyoainishwa.
HESLB imetoa masharti au vitu vya kuzingatia ambapo moja ya jambo moja ambalo limeonekana kuwashangaza wengi ni sharti namba saba ambalo limeeleza kuwa, kama mzazi/mlezi wa mwombaji anamiliki biashara, ni Meneja au Mkurugenzi wa biashara inayotambuliwa na mamlaka ya mapato au mamlaka za usajili, hatapewa mkopo.
Kigezo hicho kimewashtua wengi na kueleza kwamba, kuna baadhi ya wazazi au walezi wanatambuliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa vile wana namba ya utambulisho ya mlipa kodi (TIN) lakini kipato chao ni kidogo. Wengi waliotoa maoni kuhusu kigezo hicho wameshauri HESLB kutoa maelezo ya kina ili kuondoa utata uliojitokeza.
Mbali na kigezo hicho, vigezo vingine ni pamoja na kuzingatia muda wa utumaji maombi ambapo, huduma ya upokeaji maombi imefunguliwa Mei 10, 2018 na dirisha hilo litafungwa Julai 15.
Mbali na hilo ni kuhakikisha kuwa taarifa na nyaraka zitakazoamnatanishwa wakati wa uombaji wa mikopo kuwa sahihi na halali, kwani kutoa taarifa za uongo au nyaraka zisizo halali ni kosa kishera.
Hapa chini ni vigezo hivyo vilivyotolewa na HESLB;