Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus M. Wambura amefanya mabadiliko madogo kwa Wakuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani.
Amemhamisha Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Ramadhani Ng’anzi kutoka Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabaarani Tanzania kwenda Makao Makuu ya Upelelezi Dodoma kuwa Mkuu wa Kitengo cha Makosa ya Maadili ya Jamii.
Nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) William Mkonda ambaye alikuwa Mkuu wa Usalama Barabarani Kanda Maalum Dar es Salaam.
Pia amemhamisha aliyekuwa Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Boniphace Mbao kutoka Dodoma kwenda kuwa Mkuu wa Usalama Barabarani Kanda Maalum Dar es Salaam.
Aidha, aliyekuwa Mkuu wa Elimu kwa Umma Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Michael Deleli amemhamishia Makao Makuu ya Polisi Dodoma kuwa Kaimu Mkuu wa Maadhimisho ya Kitaifa.
Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Nassoro Sisiwaya aliyekuwa Mkuu wa Operesheni Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania amemhamishia Mkoa wa Kilimanjaro kwenda kuwa Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Kilimanjaro.