Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Camilius Wambura amefanya ziara chini Thailand na kutembelea kituo cha simu za dharura jijini Bangkok kinachohusika na kupokea, kuchakata na kusambaza taarifa za Uhalifu, Wahalifu na Majanga mbalimbali.

IGP Wambura akiwa ameambatana na ujumbe wake nchini humo ametembelea kituo hicho kwa na lengo la kujionea teknolojia inayotumika, utendaji kazi na utatuaji wa changamoto zinapojitokeza ikiwa na nia ya kujifunza na kubadilishana uzoefu kati ya Jeshi la Polisi Tanzania,Jeshi la Polisi Thailand na Polisi Bavaria ya Ujerumani ikiwa ni maandalizi ya kuelekea kwenye programu ya Miji Salama.

Please follow and like us:
Pin Share