Na Abel Paul wa Jeshi la Polis -Dar es Salaam
Aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (mstaafu,) Tanzania IGP Said Ally Mwema jana june 23,2023 amezindua kitabu alichokiandika chenye Sura Tisa na kichwa cha habari kisemacho POLISI,UTAWALA NA USIMAMIZI WA SHERIA MKAKATI WAKUBADILISHA Mwelekeo.(POLICE ADMINISTRATION & LAW ENFORCEMENT IN TANZANIA. A STRATEGIC TRANSFORMATION PERSPECTIVE).
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo ambao umefanyika katika Hotel ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam alikuwa Mhe.Jumanne Sagini Mbunge na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Aidha wageni mbalimbali walihudhuria katika uzinduzi huo ni Mwakilishi wa Ubalozi wa Ujeruma, Othman Chande Jaji Mkuu mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya Haki Jinai.
Wengine waliokuwepo ni pamoja na Katibu Kiongozi mstaafu Ombeni Sefue,Mkuu wa Jeshi la Polisi mstaafu IGP Ernest Jumbe Mangu na wajumbe wengine toka Tume ya Haki Jinai na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Hanns Seidel Foundation Mhe.Karl-Peter Schöndorfich,Rais mstaafu wa Jeshi la Polisi jimbo la Bavaria Wolfgang na Maafisa wa Polisi kutika Royal Thai Police Thailand.
Pia alikuwepo Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Hamad Khamis Hamad,Kamishna wa Utawala na Menejimenti ya raslimali watu CP Suzan Kaganda ambaye alimwakilisha Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania,
Aidha wageni wengIne waliokuwepo katika zoezi hilo ni Wanafamilia ya IGP Mstafu SAID ALLY MWEMA ,Makamishna wastaafu,Askari Polisi wa vyeo mbalimbali pamoja na watu mbalimbali.
Waliofanya uchambuzi (penalists) wa kitabu hicho mbele ya wageni ni Dr.Hildebrand Shayo,Prof.Semboja na Kamishna wa Polisi Suzan Kaganda.
Wakati akiongea na wageni waalikwa IGP Mwema alisema kwa kuwa alizaliwa miongoni mwa Watanzania,akakuwa miongoni mwa watanzania akasomeshwa na watanzania,akapewa fursa ya kujipatiwa maarifa na uzoefu na watanzania,kitabu hicho ana kitoa kwa watanzania na kitasambazwa bure kwa watanzania kwani hata maandalizi yake amefadhiliwa.
Mwisho alilishukuru Shirika lisilo la kiserikali la Hanns Seidel Foundation (HRS)kwa kufadhili uchapishaji wa kitabu hicho.