Takriban watu 95 wamethibitishwa kufariki na wengine 130 kujeruhiwa baada ya tetemeko kubwa la ardhi kupiga eneo la milima la Tibet Jumanne asubuhi, vyombo vya habari vya Serikali ya China vinasema.

Tetemeko la ardhi lililokumba mji mtakatifu wa Tibet wa Shigatse lilikuwa na ukubwa wa 7.1 na kina cha kilomita 10 (maili sita), kulingana na data kutoka Geological Survey ya Marekani. Mitetemeko pia ilisikika katika nchi jirani ya Nepal na sehemu za India.

Shigatse unachukuliwa kuwa moja ya miji mitakatifu zaidi ya Tibet. Ni eneo la jadi la Panchen Lama, mtu mkuu katika Ubuddha huko Tibet ambaye mamlaka yake ya kiroho ni ya pili baada ya Dalai Lama.