Takriban watu 78 wamefariki dunia baada ya feri kupinduka kwenye na kuzama katika Ziwa Kivu, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, umbali wa mita mia chache tu kutoka ilipopelekwa.

Feri hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka mji wa Minova huko Kivu Kusini na kuzama ilipokuwa ikiwasili kwenye ufuo wa Goma siku ya Alhamisi asubuhi.

Video inayosambaa mtandaoni inaonyeshamashua ikiinamia upande mmoja na kisha kuzama.

Kulikuwa na abiria 278 ndani yake, kulingana na gavana wa mkoa.

“Itachukua angalau siku tatu kupata idadi kamili, kwa sababu bado miili yote haijapatikana,” Gavana Jean Jacques Purisi aliliambia shirika la habari la Reuters.

Mwanaharakati wa eneo hilo, Aaron Ashuza, ambaye alikuwa katika eneo la tukio, ameiambia BBC kwamba aliona miili ikitolewa nje ya mto na kwamba majeruhi wamepelekwa hospitalini.

Takriban watoto wawili walifariki baada ya kupelekwa hospitalini baada ya ajali hiyo, kulingana na AFP.

Akizungumza kutoka kwenye kitanda chake hospitalini, manusura wa umri wa miaka 51 Alfani Buroko Byamungu, aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba hali ya maji ilionekana “tulivu”.

Aliongeza: “Niliona watu wakizama, wengi wakaingia chini. Niliona wanawake na watoto wakizama kwenye maji, na mimi mwenyewe nilikuwa kwenye nikielekea kuzama, lakini Mungu alinisaidia.”

Please follow and like us:
Pin Share