Mahakama ya Kimaitaifa ya ICC imetoa waranti ya kukamatwa kwa waziri wa zamani wa ulinzi wa Urusi, Sergei Shoigu na jenerali wa juu, Valery Gerasimov, wanaodaiwa kuhusika na uhalifu katika vita vya Urusi Ukraine.

Shoigu aliondolewa kwenye wadhifa wake wa waziri wa ulinzi mwezi uliopita, na kuteuliwa kuwa katibu wa baraza la usalama la Urusi lenye  nguvu kubwa, katika mabadiliko muhimu zaidi kufanywa na Rais wa Urusi Vladimir Putin tangu kuanza kwa vita mwaka 2022.

Mahakama ya ICJ yatazamiwa kutoa uamuzi kuhusu vita vya Gaza

Taarifa ya ICC kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa majaji wamebaini kuwa pasi na shaka washukiwa hao wawili wamehusika katika mashambulizi yaliotekelezwa na jeshi la Urusi, dhidi ya miundombinu ya umeme ya Ukraine kati ya Oktoba 10, 2022 hadi Machi 9, 2023.