Siku moja baada ya watu 121 kukanyagana hadi kufa katika hafla ya kidini katika jimbo la kaskazini mwa India la Uttar Pradesh, familia za baadhi ya waathiriwa bado zinawatafuta wapendwa wao.

Tukio hilo lilitokea wakati wa satsang (tamasha ya kidini ya Kihindu) iliyoandaliwa na mhubiri anayejiita Bhole Baba.

Polisi walisema kuwa msongamano mkubwa wa watu katika ukumbi huo katika wilaya ya Hathras ulisababisha watu wengi kukumbwa natukio hilo siku ya Jumanne , wamefungua kesi dhidi ya waandaji wakuu wa hafla hiyo.

Ni mojawapo ya majanga ambayo yamekuwa yakitokea kwa miaka mingi nchini India, ambapo ajali zinazohusisha umati mkubwa mara nyingi hulaumiwa kwa hatua za usalama na usimamizi.

Siku ya Jumatano, idadi kubwa ya polisi walikuwepo wanasiasa walipotembelea eneo hilo ili kujua jinsi mkasa huo ulivyotokea.

Makumi ya wafanyakazi walikuwa na shughuli nyingi wakiondoa hema iliyokuwa imetanda kutoka kwa eneo la tukio, karibu mita 500 kutoka barabara kuu.

Please follow and like us:
Pin Share