Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter amewatupia kijembe Chama Kikuu cha Upinzania CHADEMA, kutokana na kumteua mgombea wa Ubunge jimbo la Siha Mkoa Kilimanjaro kwenye uchanguzi mdogo unatarajiwa kurudiwa baada ya mbunge wa zamani kuhamia CCM na kupoteza sifa ya kuwa Mbunge.
Humphrey ameandika katika ukurasa huo kuwakejeli wagombea wa Upinzani waliopigwa stop kushiriki katika chaguzi za majimbo ya Longido, Singida Kaskazini na Songea mjini huku akishangaa kuona CHADEMA ikisimamisha mgombea katika jimbo la hai.
“Natafakari, wagombea waliokataliwa kugombea kupitia CDM Singida Kaskazini, Songea Mjini na Longido sijui wanajisikiaje kusikia Mwenzao wa SIHA anachukua fomu tar 19/1/18. Hasara ya kuwa na Chama kisichoheshimu Usawa wa Binadamu. Kataa kukomazwa Kikamanda wakati wenzio wanapeta ” Polepole aliandika.
kamati ya utendaji ya Wilaya ya Siha iliyoketi juzi imefanya uteuzi wa awali na kumteua Elvis Mossi kugombea ubunge jimbo la Siha ambaye sasa atashindana na aliyekuwa mbungea wa jimbo hilo kupitia chadema, Dk Godwin Mollel sasa atagombea kupitia chama cha Mapinduzi(CCM).