Baada ya kuimarisha huduma mbalimbali ikiwemo kuweka puto Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa watu wanaopenda kupungua uzito sasa huduma hii pia imeanza kutolewa MNH-Upanga.
Hayo yamezungumzwa mwishoni mwa wiki na Daktari Bingwa Mbobezi wa Upasuaji Mfumo wa Chakula, Ini na Mbobezi wa Upasuaji Kutumia Matundu Madogo MNH, Dkt. Kitembo Salum Kibwana na kusisitiza kuwa lengo ni kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma hiyo.
Dkt. Kitembo amesema kuwa mwishoni mwa wiki hii tayari mtu mmoja amepata huduma hiyo MNH-Upanga ambapo MNH-Mloganzila watu 150 wameishahudumiwa tangu kuanzishwa kwa huduma hiyo mwishoni mwa mwaka jana 2022.