Kombe la Dunia

Raia waliruhusiwa kulitazama kombe hilo likiwa ndani ya sanduku la kioo katika ikulu, Nairobi siku ya Jumatano. Wengi walitumia simu zao kupiga picha, kujiwekea kumbukumbu.

Kombe la Dunia

Kombe la Dunia

Uhuru Kenyatta

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alilipokea rasmi kombe hilo la dhahabu katika ikulu ya Nairobi Jumanne. Ni rais huyo pekee aliyeruhusiwa kuligusa pekee nchini Kenya. Kando na marais, ni wachezaji waliowahi kushinda kombe hilo pekee ambao huruhusiwa kuligusa.

Kenyatta

Uhuru Kenyatta

Uhuru Kenyatta

Kombe la Dunia

Baadhi walitumia fursa hiyo kupiga picha zao kwa kutumia simu.

Uhuru Kenyatta

Wakenya wamejitokeza kwa wingi kulitazama na kupiga picha na Kombe la Dunia la Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) ambalo limekuwa nchini humo kwa siku mbili.

Kombe hilo linatembezwa mataifa mbalimbali kabla ya michuano ya Kombe la Dunia kuanza Juni nchini Urusi.

Ni mara ya tatu kwa kombe hilo kuwa Kenya, awali ikiwa 2010 na 2013 katika ya fainali zilizofanyika Afrika Kusini na Brazil.

Mwaka 2010, lilipokelewa na rais wa wakati huo Mwai Kibaki ambaye alistaafu mwaka 2013.

Kenya ni ya 21 mwaka huu kuwa mwenyeji wa kombe hilo mwaka huu kati ya mataifa 51 yanayotarajiwa kulipokea kabla ya Juni.

Kombe hilo ambalo lina uzani wa kilo 6.1 limeelekea Maputo, Msumbiji.

Wakati wa kuwasili kwa kombe hilo Jumanne, wacheza ngoma waliovalia mavazi ya kitamaduni ya jamii ya Wamaasai walikuwepo kuwatumbuiza wageni.