MVUA kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam na sehemu mbalimbali nchini zimeleta adha kwa wakazi wake ambapo mvua hizo zilizoanza kunyesha alfajiri leo zilisababisha foleni nyingi katika maeneo mbalimbali hasa eneo la Jangwani.
Mbali ya foleni pia mvua hizo zimesababisha mafuriko maeneo mengi ambayo mtandao huu umeyashuhudia katika bonde la Mkwajuni na Jangwani yaliyokuwa yamefurika kwa maji na tope, hali iliyosababisha watembea kwa miguu wanaotokea maeneo ya Kariakoo na mengine katikati ya jiji hilo kupita kwa tabu sehemu hizo.