Na John Francis Haule, JamhuriMedia, Arusha

Kila ifikapo Februari 5 kila mwaka CCM huazimisha kumbukizi ya kuundwa kwake ambako kulifanyika mwaka 1977. Hivyo huu mwaka 2025 CCM ina timiza miaka 48 tangu kuasisiwa kwake. Na kwa kipindi hichi chote CCM imeendelea kuaminika na umma wa wa Tanzania kwa kukipa ridhaa ya kushika dola.

Japo kumeshuhudiwa vipindi vya ushindani sana wakati wa kampeni lakini CCM ina mizizi ambayo vyama vingine bado havijaweza kuitikisa. Ushindani wa CCM na vyama vingine ni wa hoja za majukwaani lakini kwenye sanduku la kura hakuna ushindani kwa kuwa CCM ina mtaji mkubwa wa wafuasi na wanachama wake ambao wakieenda kupiga kura ina pelekea ushindi wa CCM kuwa rahisi mbali na hoja za kisera na mitazamo.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Stepen Wasira ni kwamba CCM ina wanachama milioni 12.5 ambao kila mmoja akileta mtu mmoja CCM inakuwa na kura za kuanzia milioni 25. Hivyo CCM bado ina uhakika wa kushinda kila msimu wa kushika dola.

AZIMIO LA ARUSHA

Mnamo mwaka 1967 kuli pitishwa azimio na Halimashuri Kuu ya TANU uliofanyikia Arusha.

Likiwa na ajenda kuu ya kupitisha falsafa ya kuondoa unyonge wa binadamu na kumkomboa mtu mweusi kutokana na unyonyaji wa kibeberu na kuondoa matabaka.

MISINGI YA AZIMIO LA ARUSHA 1967

Msingi wa Azimio la Arusha ilikuwa ni usawa wa binadamu, utu wa binadamu, ujamaa na kujitegemea (sisasa ya ujamaa na kujitegemea uchumi dola (vyanzo vyote vya uchumi vili milikwa na Serikali centralize economy)

Misingi hii ya Azimio la Arusha ambayo ilipitishwa na Halimashauri Kuu ya TANU baadae 1977 baada ya TANU na ASP kuungana na kuunda CCM ililithi misingii hii ya Azimio la Arusha.

Je? Mpaka sasa CCM inaiishi hii misingi ya Azimio la Arusha? Jibu ni ndio kuwa CCM bado inaamini katika misingi hii ya Azimio la Arusha

Moja; Utu wa binadamu, sote ni mashahidi kuwa CCM imekuwa kipaumbele kutetea utu na heshima ya mtu mbali na mitazamo kinzani ya ideolojia lakini utu wa mtu ndio kipaumbele cha CCM, mfano CCM kupitia katibu mwenezi CPA Makala aliendesha mchango wa kutengeneza gari ya Tundu Lissu ambaye kwa sasa ni mwenyekiti wa CHADEMA.

Kwa hili ni uthibitisho tosha kuwa CCM inaamini katika misingi ya Azimio la Arusha.
Mbili, usawa wa binadamu, binadamu wote ni sawa CCM inaamini katika usawa wa binadamu mfano katika sera ya elimu iliyozinduliwa hivi karibuni ni kwamba elimu ni bure ngazi ya msingi mpaka sekondari. Usawa kwenye ajira na fursa zote zinazopatikana nchini.

Tatu, udugu wa binadamu, viongozi wote wa CCM huitana ndugu hivyo CCM ni kama familia moja yenye ideolijia au itikati inay randana na kuifanya iwe mfano wa chama kikubwa cha siasa na madhubuti barani Afrika na Duniani.

Nne, Uchumi dola. Kwa kuwa CCM ni chama cha siasa kinachosoma ala za nyakati na kwenda na mawimbi na uchumi wa dunia kuna baadhi ya misingi kiliona ni vema kikaachia sekta binafsi ifanyekazi kwa sera ya ubinafsishaji japo kuna misingi bado kinaiongoza mfano reli ni mali ya serikali. Mashirika ya umma mfano Shirika la Posta, Shirika la Umeme (TANESCO).

Tano, falsafa ya siasa za ujamaa na kujitegemea (self reliand) ili kuodoa unyonge wa binadamu kama iliyo afikiwa kwenye Azimio la Arusha ni muhimu kwa taifa kujitegemea mfano bajeti ya 2024/2025 ya Serikali ina uwezo wa kutegemea makusanyo ya kodi ya ndani kwa asilimia 70 haya ni mafanikio makubwa sana na hata uchaguzi unagharamiwa na fedha za ndani hii inathibitisha kuwa CCM bado inaiishi misingi ya Azimio la Arusha.

Ni ukweli usiopingika kuwa misingi ya Azimio la Arusha imewezesha taifa letu kuwa moja kwa kuwa liliweka mazingira ya kuodoa utabaka, ukabila, mfano shule na taasisi zilitaifishwa kwa maslahi ya wananchi wote ‘Nationalization policy’ hivyo sisi wananchi hatuna budi kuendelea kukiamini Chama cha Mapiduzi kueendelea kushika dola na kuongoza serikali.

Mwandishi ni Mkuu wa Soko Kuu la Arusha, 0756717987 au 0711993907