Na Magrethy Katengu,JamuhuriMedia,
Dar es Salaam

Bodi ya Mikopo Tanzania (HELSB), imewaomba wananchi kuwafichua wanufaika wa mikopo walio na vipato na kazi ambao mpaka sasa wamekaidi kurejesha fedha hizo ili kusaidia wanavyuo wengine nao waunufaike.

Ombi hilo limetolewa leo Juni 28,2024 Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya mikopo ya elimu ya juu nchini (HELSB), Dkt Bill Kiwia,amesema wakati wa uzinduzi wa kampeni fichua “kuwa Hero wa madogo” itakayoendeshwa kwa miezi miwili na itakuwa ya kizalendo.

Amesema kuwa kila mtu ambaye anamfahamu mnufaika wa mikopo hiyo na ana kipato au ameajiriwa na taasisi, kampuni ataombwa kutoa tarifa ya huyo mhusika kwa kutuma majina yake yote matatu,Chuo kikuu alichosoma na mahali alipo ili afuatiliwe.

” Tunafahamu kuwa wateja wetu wadaiwa sugu ni wengi wengine wameajiriwa na taasisi binafsi, makampuni huku wengine wakiwa wamejiajiri na wanavipato hawakumbuki fadhila walizotendewa wakiwa masomoni kupewa mikopo wakiwa vyuoni lakini hawataki kurejesha fedha hizo ni.hivyo kampeni hii tunawaomba ushirikiano wananchi wote tusaidiane kuwafichua ili wengine nao wanufaike”amesema Dk Kiwia

Sanjari na hayo amebainisha kuwa hali ya urejeshwaji mikopo ni nzuri ambapo kwa sasa wanakusanya bilioni 15 kwa mwezi sawa na 70% ikilinganishwa miaka iliyopita hivyo kupitia kampeni hiyo ya itasaidia kupunguza malalamiko kwa baadhi ya wanavyuo kusema boom wanalopewa haliwatoshi kulingana hali ya maisha .

Sanjari na hayo kiasi wanachokidai kikubwa trilon 2.1 na hadi sasa zaidi wamekusanya trilion 1.3 bado bilioni 600 hivyo kupitia kapeni hiyo f wanazotarajia wanafunzi elfu 50 kukusanya kiasi cha bilioni 200.

Aidha wito umetolewa kwa mama,kaka,dada na wanafunzi ambao walishawahi kunufaika na mikopo ya elemu juu kuwa wazalendo kuwafichua wale ambao hawajarejesha kwa kutuma ujumbe kwa simu no,0739665533, kupiga simu 0736665533 wakituma majina yao matatu vyu vyuo walivyosoma na mahali walipo kwa sasa hii isaidie wengine nao wanufaike kwani kuna wanafunzi wasio na wazazi wote wawili , wengi familia zao vipato duni wameshindwa kusoma kwa kukosa ada .

Kwa upande wake,Mkurugenzi urejeshaji na urejeshwaji mikopo CPA George mziray ,amesema wanafunzi wote waliohitimu kidato cha sita na wanahitaji kwenda vyuoni dirisha la mikopo limefunguliwa waombe kupitia mtandao