Na Isri Mohamed
Mshambuliaji wa Fountain Gate FC, Ditram Adrian Nchimbi ‘Duma’, amepata dili la kusajiliwa na klabu ya Etincelles inayoshiriki ligi kuu ya Rwanda.
Nchimbi yupo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha uhamisho wake kujiunga na klabu hiyo.
Nchimbi mwenye umri wa miaka 30, ameingia mkataba wa miezi sita kuanzia Januari hadi june 2024.
Ditram Nchimbi amewahi kuzichezea klabu mbalimbali za ligi kuu hapa nchini hapa nchini ikiwemo Mbeya City, Azam fc, Polisi Tanzania na Yanga sc.