Na Isri Mohamed

Aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni na baadaye Ubungo, Dar es Salaam Boniface Jacob (Boni Yai), amepatiwa dhamana inayoendana na masharti yatakayowekwa kwenye shauri la msingi, ambalo sasa linaendelea.

Dhamana hiyo imetolewa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu leo Oktoba 07, 2024 baada ya kukubaliana na hoja za utetezi kuhusu pingamizi la kutopatiwa dhamana lililokuwa limewekwa na Jamhuri (serikali).

Maamuzi hayo madogo ndani ya kesi ya msingi yametangazwa Mahakamani hapo na Hakimu mkazi Mkuu Franco Kiswaga wa Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam ambapo shauri hilo lililetwa Mahakamani hapo kwa ajili ya kusomwa hukumu ya kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi.

Please follow and like us:
Pin Share