Na Mwamvua Mwinyi, JamhuriMedia, Kibaha
Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha kwa Kushirikiana na Taasisi ya Anjita Child Development Foundation imefanya uzinduzi wa program Jumuishi ya Taifa ya Malezi ,Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto (MMMAM).
Uzinduzi huo umefanyika kwa kushiriksha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, kisiasa , sekta binafsi, wataalam mbali mbali kutoka Halmashauri na wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo.
Program hiyo inaongozwa na kauli mbiu Mtoto kwanza na watoto wetu tunu yetu.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo kaimu Mkurugenzi Fatuma Kisalazo amesema programu hiyo itasaidia kumkuza mtoto kimwil ,kiakili, lugha, kijamii, kiutamaduni, kihisia na kimaadili.
Aidha Kisalazo ameongeza kwamba programu hiyo inalenga kutoa huduma za afya , lishe, malezi yenye mwitikio, ujifunzaji wa awali na ulinzi na usalama wa watoto wenye umri wa miaka 0 -8 kuimarisha ushirikiano wa wadau wa sekta mbalimbali katika huduma za programu.
Kisalazo pia ameikumbusha jamii kuwa jukumu la kulea watoto na kuwalinda ni la jamii nzima wazazi walezi, serikali na wadau wote.
Afisa ustawi wa jamii bwana Yahya Mbogolume amewataka wazazi kutimiza majukum yako ya kimalezi sqmbamba na wazazi kushiriana na walimu kufuatilia maendeleo ya watoto wao wanapokua mashuleni.
Mmoja wa wadau walioshiriki uzinduzi huo Stephano amesema programu hiyo ni nzuri na itasaidia kuokoa taifa.
Stephano ameishauri serikali kukaa na wamiliki wa vituo na kuzungumza nao kwani wanamengi kutoka kwa watoto wanaowalea lakini wanashindwa kuyatoa kutokana hawana ushahidi wa kutosha.
Naye Deodan Katie amesema watoto wengi wanaharibika kutokana na vipindi vilivyo kwenye runinga havina maadili kwa watoto.
Pia ameshauri watoto wapewe elimu ya kujielewa na wajengewe kujiamini ili wanapokutana na changamoto waweze kuripoti.
Nae Mkurugenzi wa Taasisi ya Anjita Child Development Foundation amesisitiza wadau kufanya kazi kwa kushirikiana, kutoa taarifa za utekelezaji na kuhimiza wadau na serikali katika kutenga bajeti za shughuli za Malezi Makuzi na Maendeleo ya Mtoto.