Meya Mwita azitaka halmshauri za jiji la Dar es Salaam, kuajiri watumishi kwa ajili ya kuzika watu wasiokuwa na ndugu.
MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amezitaka halmashauri zote jijini hapa kuajiri watumishi ambao watakuwa wanafanya kazi ya kuzika miili ya watu ambao watabainika kuwahawana ndugu.
Meya Mwita ametoa kauli hiyo jijini hapa leo kwenye kikao cha robo ya pili ya Baraza la Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam ,ambapo amewaeleza madiwani hao kuwa jukumu la kuzika marehemu wasiokuwa ndugu ni la jiji,kwakushirikiana na halmashauri hivyo wanapaswa kuwajibika katika hilo.
Amefafanua kuwa hadi sasa jiji limeshanunua gari pamoja na mahitaji mengine ya kuhifadhia miili hiyo pindi inatokea na kwamba changamoto iliyopo ni watu ambao watashirikiana kutekeleza jukumu hilo.
“ Mtakuabliana na mimi kwamba tulishakubaliana kwamba jambo hili lifanyike kwenye halmashauri zetu, lakini hadi sasa Kinondoni pekee ndio wametimiza agizo hili, sasa ninaagiza tena halmashauri nyingine za jiji hili kuajiri watu hao” amesema Meya Mwita.
Mwita amesema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na halmashauri nyingine zilizopo jijini hapo walikubaliana kuzika watu wasiokuwa na ndugu hivyo kila mmoja anapaswa kutekeleza makubaliano hayo.
“Hivyo marehemu wanapokuwa wamekaa muda mrefu wanalazimika kuzikwa na jiji, natulikubali kuchangia usafiri,dawa na sanda,” amesema.
Amefafanua kuwa watu wasiokuwa na ndugu wanapokufa, wanapokaa hospitalini zaidi ya siku 20,jiji linalazimika kuwazika hivyo wapo ambao wanazikwa kwenye halmashauri mbalimbali.
Hivyo wakati Jiji la Dar es Salaam likitimiza wajibu wake katika kuzika marehu hao kila halmashauri linajukumu la kutoa watumishi kwa ajili ya kuzika.
Amefafanua taarifa alizonazo ni Halmashauri ya Kinondoni pekee ndio ambayo imeajiri watumishi kwa ajili ya kuzika miili ya watu ambao wamefariki na hawana ndugu.
“Ni wajibu wa halmashauri kuhakikisha wanafanikisha kupatikana kwa watumishi hao haraka,” amesema Meya Mwita.
MWISHO
Imetolewa leo Machi 22 na Christina Mwagala,Afisa Habari Ofisi ya Meya wa jiji.
Mstahki Meya wa jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita akiongoza kikao cha robo ya pili ya baraza la madiwani leo, kushoto ni Mkurugenzi wa jiji Sipora Liana.
Px. 2. Madiwani wa jiji la Dar es Salaam,wakifuatilia kwa umakini hoja mbalimbali zinazotolewa na wajumbe wengine ambao ni madiwani wa baraza hilo.
Px3.Diwani wa Kata ya Mbagala Kibonde Maji, Abdala Mtinika a kitoa hoja mbele ya baraza la madiwani lililofanyika leo katika ukumbi wa karimjee.
Px. 4 Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akifuatilia kwa umakini michango inayotolewa na wajumbe wa baraza hilo.kushoto ni Mkurugenzi wa jiji Sipora Liana.
Px.5 Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akisisitiza jambo kwenye mkutano wa baraza la madiwani uliofanyika leo katika ukumbi wa karimjee.