Gwiji wa Manchester United, Bryan Robson, maarufu kwa jina la “Captain Marvel,” leo anaongoza kundi la wasafiri 23 katika safari ya ajabu ya kupanda mlima mrefu zaidi barani Afrika, Mlima Kilimanjaro.


Safari hiyo, ambayo itashuhudia kundi hilo likikwea mita 5,895 juu ya usawa wa bahari, inalenga kukusanya fedha muhimu kwa ajili ya Wakfu wa Manchester United, kusaidia elimu na programu zake za kufikia jamii.

Kundi hilo liliondoka Uwanja wa Ndege wa Manchester Jumapili mchana na kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro mkoani Kilimanjaro jana kwa siku saba zijazo litapitia maeneo yenye changamoto nyingi, ikiwamo misitu yenye miti mirefu, miinuko na jangwa la nyanda za juu, kabla ya kufika ukanda wa Arctic kwenye kilele.

Please follow and like us:
Pin Share