Rais Ebrahim Raisi alikuwa karibu kufikia nafasi ya juu ya madaraka katika Jamhuri ya Kiislamu na alipendekezwa sana kupanda hadi nafasi hiyo.
Kufariki ghafla kwa Rais Ebrahim Raisi katika ajali ya helikopta siku ya Jumapili kumezua gumzo la nani hatimaye atachukua nafasi ya kiongozi mkuu Ayatollah Ali Khamenei mwenye umri wa miaka 85 ambaye afya yake imekuwa ikifuatiliwa na wengi kwa muda mrefu.
Hatima mbaya ya rais wa Iran mwenye misimamo mikali haitarajiwi kuvuruga mwelekeo wa sera ya Iran au kuitikisa Jamhuri ya Kiislamu kwa njia yoyote ile.
Lakini itakuwa majaribu kwa mfumo ambao watu wenye msimamo mkali wa kihafidhina sasa wanatawala maeneo yote ya mamlaka, waliochaguliwa na ambao hawajachaguliwa.
Wapinzani wake watafurahishwa na kuondoka kwa mwendesha mashtaka wa zamani anayeshutumiwa kwa jukumu muhimu katika mauaji makubwa ya wafungwa wa kisiasa katika miaka ya 1980 ambayo alikanusha; watatumaini mwisho wa utawala wake utaharakisha mwisho wa utawala huu.
Kwa wahafidhina watawala wa Iran, mazishi ya serikali yatakuwa tukio lililojaa hisia; pia itakuwa fursa ya kuanza kutuma ishara zao za mwendelezo.
Nafasi nyingine muhimu ambayo lazima ijazwe ni nafasi ya kiongozi huyo kwenye Bodi ya Wataalamu, ambayo ina mamlaka ya kuchagua kiongozi mkuu mpya, wakati mabadiliko hayo muhimu zaidi yatakapowadia