Klabu ya YangaSC leo Septemba 12, 2022 imesaini mikataba mipya miwili na wadhamini wao GSM, mkataba wa kwanza ni wa udhamini wa uzalishaji na usambazaji jezi na vifaa mbalimbali wenye thamani ya shilingi bilioni 9.1 kwa muda wa miaka mitano.
Mkataba wa pili ni udhamini wa haki za kuweka nembo ya GSM Foam kwenye jezi za klabu hiyo wenye thamani ya shilingi bilioni 1.8 kwa muda wa miaka mitano.