Ndoa ya Geita Gold na straika kinara wa mabao wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara uliopita msimu uliopita, George Mpole, imefikia tamati hii leo baada ya pande hizo mbili kukubaliana kuvunja mkataba kwa maslahi ya kila upande. Taarifa ya Geita Gold imeeleza kwamba George Mpole ni mchezaji huru kuanzia leo tarehe 07/12/2022.
Kwa taarifa hiyo ni wazi sasa klabu nyingi za ligi kuu zitapigana vibega kuwania saini mchezaji huyo ambaye hakuwa uwanjani muda mrefu katika kuitumikia klabu yake kufuatia migogoro ya kimaslahi iliyokuwa ikirindima kati ya mchezaji huyo na ‘wachimba dhahabu wa Geita’.