Na Tatu Mohamed, JamhuriMedia, Dar es Salaam

MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) imewataka wananchi kutembelea banda lao katika Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) kujionea shughuli mbalimbali wanazofanya ili kujifunza kuhusu masuala ya kemikali.

Hayo yameelezwa na Mwakilishi wa GCLA, Stafford Maugo katika banda lao lililopo katika Viwanja vya maonesho hayo yanayoendelea jijin Dar es Salaam.

Amesema kupitia maonesho hayo watawaelezea aina ya chunguzi wanazofanya kwa kushirikiana na taasisi binafsi na serikali.

“Tutawapa elimu ya vitu mbalimbali, kwa mfano polisi akikamata dawa za kulevya, bangi na mirungi atazileta hapa kwenye maabara ya rufaa kwaajili ya kufanya uhakiki kama ni kweli ni dawa za kulevya au kitu kingine,” amesema.

Maugo ambaye pia ni mkaguzi wa kemikali amesema pia kesi za ubakaji askari wanakamata vielelezo na kuvipeleka kwenye maabara ili kumfahamu muhusika.

Amesema pia kuna huduma za vinasaba wanapima ili kutatua migogoro ya familia kuhusu uhalali wa watoto.

Maugo amesema pia wanachunguza kuhusu jinsi tata kwa watoto waliozaliwa na jinsia mbili lengo ni kusaidia madaktari kutambua jinsi iliyotawala.

“Vipimo hivyo vitamsaidia daktari kuondoa ile jinsi ambayo haijatawala,” amesema Maugo.

Amesema katika maonesho hayo wanawasiaida wateja wa kemikali kujisajili na kuingia kwenye mfumo wa maalum wa huduma za kemikali.
Amesema wadau wote wa kemikali wanatakiwa kujisaili na wanapeleka napetwa kuunga.

Please follow and like us:
Pin Share