TFS inamuunga mkono vyema Rais Samia kulinda mazingira kupitia upandaji miti.
Afisa Tarafa wa Tarafa ya Katerero iliyopo Bukoba mkoani Kagera Ndugu Bwanku M Bwanku leo Jumatano Mei 29, 2024 amepokea jumla ya miche ya miti 500 kutoka kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya Bukoba kwa ajili ya kupanda katika maeneo mbalimbali kwenye Tarafa yake ili kuunga mkono harakati za Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Muungano na Mazingira kupanda miti ili kulinda mazingira.
Gavana Bwanku amepokea miche hiyo katika Kitaru cha TFS kilichopo Kata ya Katoma ambapo ameipongeza sana TFS kwa jinsi wanavyotekeleza kwa vitendo adhima ya Rais Samia kulinda mazingira kupitia upandaji miti kwa kuzalisha miche ya miti ya kuigawa ili kupandwa kwenye maeneo mbalimbali.
Kwa sasa Tanzania na Dunia imekua kwenye tishio la ukataji miti na uharibifu wa mazingira, hivyo ni jukumu la kila mmoja kupanda miti kwa kasi kukabiliana na tishio hili baya kwa maisha.