Na Isri Mohamed, JamhuriMedia, Dar ea Salaam
Mtu mmoja amefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha gari aina ya fuso yenye namba za usajili T 195 EDF, iliyokuwa imebeba watumishi wa shirika la umeme Tanesco.
Gari hilo lililokuwa likitokea Igowole kuelekea mafinga limepata ajali katika eneo la Majinja.
Chanzo cha ajali inaelezwa kuwa dereva wa gari ya TANESCO alikuwa anamkwepa mwendesha baiskeli ambaye alikuwa akitokea upande mwingine wa barabara
Majeruhi wote wamepelekwa katika hospital ya Mji wa Mafinga kwa ajili ya matibabu.