Nyota na nahodha wa timu ya Singida Foutain Gate, Gardiel Michael Kamagi, ametimkia zake kwa Madiba nchini Afrika Kusini kujiunga na timu ya Cape Town Stars kwa mkataba wa miaka miwili.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Rais wa Singida FG, Japhet Makau amesema Gardiel ameshaondoka nchini kuelekea Afrika kusini kujiunga na klabu hiyo.
Gardiel mwenye umri wa miaka 27, ambaye anacheza nafasi ya beki wa kushoto amedumu Singida kwa msimu mmoja tu akitokea Simba.
Gardiel amewahi kwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya majaribio katika moja ya vilabu lakini hakufanikiwa kusajiliwa, Hii inakuwa ni mara yake ya kwanza kwenda kusakata kabumbu nje ya Tanzania.