“Hakuna jambo baya linalomharibu binadamu kama woga, na yeyote anayemwamini Mungu anapaswa kujisikia aibu kwa kupata woga juu ya chochote [katika dunia hii].”
Haya ni maneno ya mpigania Uhuru wa India, Mahatma Gandhi aliyoyatoa wakati akiwahamasisha Wahindi kujenga mshikamano.
***
Churchill: Tusifungue vinywa ovyo
“Sisi ni mabwana wa maneno tusiyosema, lakini ni watumwa kwa maneno yaliyotutoka hovyo [vinywani].”
Haya ni maneno ya Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Winston Churchill, alipokuwa akiwaasa Waingereza kutumia busara kabla ya kusema neno.
****
Lincoln: Uaminifu muhimu
“Nimefanikiwa [kwa kiwango hiki] leo kwa sababu nilikuwa na rafiki aliyeniamini na sikuwa na moyo wa kumwangusha…”
Haya ni maneno ya Rais wa 16 wa Marekani, aliyeongoza kati ya Mwaka 1861 hadi Aprili 1865 alipouawa. Alipata heshima kubwa duniani kwa kuhubiri upendo, amani na mshikamano. Kwa kipindi kifupi alichoongoza alifanikiwa kuzuia utumwa na biashara ya utumwa.
****
Shakespeare: Usiseme sana
“Wasikilize wengi, zungumza na wachache.”
Haya ni maneno ya mtunga mashairi maarufu duniani, William Shakespeare, akiwakemea watu wenye utamaduni wa kuzungumza maneno mengi bila kusikiliza wengine.