Naitwa Dk.  Joseph Kankola Buberwa au Dk. JK Buberwa. Ni Mtanzania mwenye umri wa miaka 50. Ni  Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya JKBRS International Co Ltd yenye ofisi zake jengo la Ubungo Plaza, Dar es Salaam.

Hivi karibuni nimependekezwa kuwa Mwenyekiti wa Muunganikano wa Wana Maono (Visionaries) duniani, tukiwa ni waanzilishi wa chama hiki.

Nimekuwa mtu mwenye maono makubwa kuhusu fursa mbalimbali za kibiashara kwa ajili ya taifa letu na kwa ajili ya Bara zima la Afrika, lakini kwa bahati mbaya nchi yangu mwenyewe haikutambua zawadi ya pekee ambayo Mungu alinipa. Kwa hiyo wakawa wananizuia na kunikwamisha nyakati zote ninapozindua miradi mikubwa, kwa hakika kama wasingenikwamisha nyakati zote nami ningekuwa miongoni mwa matajiri wakubwa katika Afrika.

Simulizi kamili ya uwekezaji wangu ambao niliwahi kufanya nchini na nje ya nchi na kwa bahati mbaya ukawa unakwamishwa na baadhi ya taasisi za serikali za nchi yangu na zilichapishwa na magazeti saba, Januari, 2017 ikiwa na kichwa: “Barua ya wazi kwa Rais Magufuli; Wazawa tunazuiwa kushiriki ujenzi wa taifa.” Habari hii unaweza kuisoma kwenye Gazeti la Uhuru la Januari 28, 2017, ukurasa wa 10 na 17 (unaweza kusoma makala hii kwenye website yetu ya www.jkbtanzania.co.tz, sehemu ya publications au ingiza link hizi kwenye simu yako utazipata makala hizo: ukurasa wa 10: https://bit.ly/2LGt0we; https://bit.ly/2XqbrHm

Nikiwa mwana maono wa kuvumbua fursa za biashara na miradi, baada ya kupitia magumu mbalimbali tangu mradi wangu mkubwa wa uzinduzi wa dawa katika maonyesho ya Sabasaba ya Julai mwaka 2016, sijakata tamaa ya kuwekeza, bali sasa chini ya uongozi thabiti wa Dk. John Magufuli na serikali yake thabiti nimeamua kurudi tena kwenye uwekezaji mkubwa kuliko uliopita nikitumaini kwa sasa serikali haitanitia tena hasara.

Nikiwa mtu wa maono, Mungu amenipatia njia nzuri sana ambayo ni ya kila mtu anayetaka kutuchangia mtaji wa kuanzishia miradi tuliyonayo, tunataka apate faida katika maisha yake yote na familia yake (WIN WIN). Kwa kweli njia ambayo nimekuja nayo, nafikiri itakuwa ni njia ya kwanza kutokea Tanzania na duniani kote. Na njia hii hakika imekuja kwa kupitia njia ngumu ya kutafakari, uamuzi, kutenda, kushindwa na kushinda.

Kwa sababu, katika mapambano ya karibu miezi saba kuanzia Januari, 2019 hadi sasa, ambayo nimepambana kwa njia nyingi ya kutafuta watu au taasisi za fedha ambazo wangeweza kukubali kuniazima mitaji au kunikopesha ili nipate pesa za kunyanyukia tena na wao wapate faida za maisha yao yote. Lakini huwezi kuamini watu wote ambao niliwafikia wanikopeshe Sh milioni 50 au 30 wote walikataa na wengine kunibeza, baadhi wakinikatia mawasiliano kabisa.

Kwa kweli kwa bahati mbaya nimekuta Watanzania wengi hawana kabisa mioyo ya kuinuana kama wenzetu wa nchi zinazoendelea. Hapa wengi unapowafikia kuomba ufadhili au mikopo, unapotoka wanakusonya na kukudharau kabisa hata kama wana pesa za kukupa. Nikagundua watu wenye mamlaka unapowafikia na wazo, si la kuwakopa pesa, bali na wazo la wao wakiwa viongozi kukudhamini kwa watu wenye pesa ili waniamini nipate pesa ya kuendesha miradi mikubwa niliyonayo ambayo itanufaisha familia zetu na taifa, lakini wakitoka hapo wanapiga simu kwa vyombo vya dola ili nichunguzwe kama akili zangu ziko sawasawa (inashangaza sana).

Na kwa kusema hivyo ni kwamba nchi yangu na watu wangu mwenyewe hawana huruma na watu ambao Mungu amewajalia uwezo wa maono (visionaries) kuhusu fursa na mambo mengine katika taifa langu. Kinachotokea badala ya kutuelewa na kutusaidia katika ndoto zetu za kuleta maendeleo ya nchi, badala yake wanatuita vichaa, wakati tumefanya mambo makubwa na yanayoonekana katika jamii, lakini bado watu wanadai huyo ni mgonjwa wa akili.

Nikijitolea mfano, mwaka jana askari Polisi walikuja na gari lao likiwa na askari wanane wakiwa na silaha wakanichukua ofisini kwangu Ubungo Plaza, wakati walikuwa wamenipigia simu kuwa ni maofisa wa Ikulu wanakuja tuzungumzie ajenda za kumuona rais, kulingana na maombi niliyotuma Ikulu. Lakini nikashangaa wananipeleka Muhimbili na kunilaza katika wodi za wenye magonjwa ya akili (Psychiatric ward) kwa nguvu, wakidai ni agizo la Rais Magufuli nitibiwe kwa sababu nina magonjwa ya akili. Nami kutokana na kuogopa serikali nilikubali kunywa dawa zao kwa muda wa miezi sita mfululizo huku nikisimamiwa.

Lakini ukweli ndugu Mtanzania, dawa hizo walizokuwa wakinipa tangu Machi 2, 2018 zilikuwa zikinizidi nguvu sana. Kwa hiyo nilikuwa mtu wa kulala ndani saa 24 nikiamka ni kula tu na kulala; wakati huo hata kusoma sms au e-mail au magazeti nikawa siwezi kabisa.

Ukitoka nje mwanga wa jua unauona kama jua linawakia machoni, salama yangu ilikuwa ni kukaa ndani. Baada ya miezi sita, walipoacha kunisimamia ndipo nilianza kufanya ujanja wa kudanganya kwamba nazimeza hizo dawa lakini badala ya kuzimeza nikawa nazitupa. Ndipo baada ya miezi mitatu ya kukwepa kuzimeza, nikaweza kuanza kupata uwezo kidogo wa kwenda ofisini angalau kwa muda wa saa moja au mbili, narudi kulala nyumbani.

 Kwa sasa namshukuru Mungu nimeanza kurudi kwenye uwezo wangu kamili wa kufanya kazi zangu, ingawa kuna athari zingine bado zinanisumbua kama kupatwa kizunguzungu cha mara kwa mara.

Mei 2019 niligundua kuwa hilo tukio lilipangwa na watu wanaonifanyia njama wakishirikiana na baadhi ya waliokuwa askari Kituo cha Gogoni, Kibamba na baadhi ya madaktari wa Kitengo cha Magonjwa ya Akili Muhimbili.

Walinituhumu kuwa nilikuwa nashika kisu na kutaka kumpasua mke wangu tumbo ili nimtoe mtoto wangu tumboni (wakati huo mke wangu alikuwa mjamzito wa mimba ya miezi minane). Pia wakadai kuwa majirani wa Kibamba, Luguruni ninakokaa pia walikuwa wamenichoka kwa sababu nilikuwa nazunguka nikipiga makelele mitaani nikijigamba kuwa mimi ni tajiri mkubwa Kibamba.

Kwa kweli matukio hayo ni mambo ya uongo. Hakujawahi kuwa na matukio hayo nyumbani, kwenye ujirani Kibamba, ofisini kwangu na kote ninakosafiri, zilikuwa njama za kutunga kunizuia nisiendeleze maono makubwa ya miradi na biashara.

Nagundua watu hao hao mwaka 2013 walinifungulia faili kwenye wodi hiyo hiyo ya magonjwa ya akili Muhimbili wakishirikiana na madaktari, kwamba nina magonjwa ya akili na wananitibia magonjwa hayo, wakati sijawahi kufanyiwa matibabu hayo ya magonjwa ya akili, bali niliwahi kuhudhuria Muhimbili kwenye kliniki ya wagonjwa wa kisukari tu, kwa sababu nimekuwa mgonjwa wa kisukari kwa miaka 12 sasa na sukari yangu haijawahi kushuka chini ya 13, mara nyingi inakuwa 20 kwenda juu, lakini hainiletei madhara kwa sababu nazingatia masharti ya dawa ninazotumia za life, dfp na s-one.

Dawa aina ya ‘life’ inanilinda mishipa ya fahamu, ubongo, misuli, moyo, figo na mifumo mingine ya mwili kujijenga kutokana na athari za kisukari na kuzuia nisipatwe na lehemu (cholesterol) isijijenge kwenye damu, kusawazisha utendaji wa kemikali mwilini na kuondoa sumu mwilini (toxins), kuzuia moyo kupanuka na faida nyingine nyingi.

Na niliishatoa ushahidi miaka ya 2008 kuwa huwa nasafiri nikiendesha gari nikiwa peke yangu na bila msaidizi kutoka Dar es Salaam hadi Zambia, Malawi, Uganda, Rwanda na Kenya mara nyingi tu na sukari yangu hapo inakuwa juu ya 33 mwanzo wa safari hadi mwisho na nikianza safari huwa sipumziki njiani hadi nifike ninakoenda. Dawa hizi naishauri sana jamii yangu kuzitumia bila kukawia; kwa sababu zimenisaidia sana mimi binafsi sukari yangu isiyoshuka, isinisumbue au kunipa madhara kirahisi.

Na kwa watu hawa wenye magonjwa ya kisukari na presha ya kupanda zinawasaidia kupunguza uwezekano wa kupatwa na kiharusi (stroke), shambulio la moyo (heart attack) na dawa kama life inadhibiti ukuaji wa bakteria kwenye damu, kwa hiyo inasaidia wagonjwa wa kisukari wanapopatwa na vidonda vipone kwa haraka, na dawa hizi si kwamba ni kwa wagonjwa tu wa kisukari na presha tu, bali watu wote kuanzia watoto hadi wazee kwa ajili ya kulinda na kujenga afya.

Dawa ya Dental Formula Power (DFP), ambayo kazi yake ni kutibu magonjwa ya meno bila kung’oa na kuyapa kinga meno na kuyafanya meno yawe imara hadi utakapoingia kaburini bila kung’oka na yakiwa imara uzeeni, kama utakuwa unatumia DFP mara moja kila baada ya miezi sita kwa maisha yako yote.

Kwa hiyo kama ningekuwa situmii DFP mara moja kila baada ya miezi mitatu na kwa jinsi sukari yangu inavyokuwa juu sana muda wote kwa hii miaka 13; ningekuwa kibogoyo. Lakini meno yangu yako imara sana na bila magonjwa kabisa. Wagonjwa wengi wa kisukari wanapata matatizo ya meno hasa magonjwa ya fizi na mwisho kulegea kwa meno na kung’oka yenyewe tu. Na wengi wanakuwa vibogoyo mapema, sasa DFP inawaepusha wasipatwe na athari hizo mbaya za meno.

Na dawa ya tatu ambayo imekuwa mkombozi wangu ili nisipofuke macho ni dawa ya Sight One (S-one) ambayo inasaidia mishipa ya macho na mboni za macho zisipoteze uwezo unaosababisha macho kupunguza uwezo wa kuona au kupofuka kabisa.

Na S-one inasaidia watu wenye umri mkubwa kuondokana na uwezakano wa kuja kuwa vipofu uzeeni. Kwa hiyo dawa hizi tatu nikiwa mgonjwa wa kisukari ndizo zinanipa jeuri kutohangaika na ugonjwa wangu wa kisukari kwa sababu zinasaidia kukarabati na kujenga afya yangu.

Kwa hiyo maadui zangu wamekuwa wanatumia vibaya hizo ripoti feki za Kitengo cha Psychiatric Muhimbili kusadikisha Ikulu na washirika wangu wa kibiashara  kuwa mimi ni mgonjwa wa akili na wakiwapa uthibitisho wa madaktari wa Muhimbili kuwa ni kweli mimi ni mgonjwa wa akili (kwa kweli sisi Waafrika kumuumiza ndugu yako kwa hila na fitina, ni jambo dogo sana, hata mtu hajali kama huyu mtu ana watu ambao wanamtegemea au mtu kama mimi nimekosa miradi mingapi kwa kutuhumiwa kwa hila na fitina hizo). Serikali yenyewe imekuwa ikishindwa kunipa ushirikiano wowote kwa sababu wana faili langu kuwa mimi ni mgonjwa wa akili. Kwa hiyo kwa serikali kila nifanyacho wanafikiri, siyo akili zangu.

Na kwa sasa baada ya kuanza upya mikakati ya kuendeleza miradi niliyonayo, nasikia kuwa watu hao hao, wanafanya jitihada zingine za kunikamata kwa nguvu nikalazwe tena kwa wagonjwa wa akili, wakidai kwamba matatizo yangu ya akili yamerudi tena kwa kasi.

Bado najiuliza maswali mengi ambayo sijapata majibu hadi sasa, kwamba wanafanya juhudi ya kunisingizia magonjwa ambayo sina na wananilaza kwenye kitengo cha Psychiatric kwa matukio ya kutunga ambayo si ya kweli, ili iweje? Na wanapata faida gani ambapo miradi yangu mikubwa kwa taifa inapokwama?

Na mbona sijawahi kudhuru mtu yeyote hata kwa kumpiga kofi au kumtukana katika jamii? Mbona sijawahi kuvua nguo au kuongea ovyo barabarani? Mbona naishi vizuri na watu wote wa hapa nchini na nje ya nchi? Mbona napatana vizuri na jamii na hata wateja wa dawa zangu na ninaishi vizuri sana na majirani zangu na watoto na familia yangu?

Nawaomba waache kunifanyia hila, ningekuwa mbali sana, wafanyakazi ambao wakati tofauti tofauti niliwaajiri kazi wapo mitaani kila siku wananiombea nifanikiwe tena warudi kazini. Waniache nitumie vizuri vipaji ambavyo Mungu amenipa,  tena kwa uhuru ili nami nishiriki kujenga uchumi wa taifa.

Ndiyo namkaribisha kila Mtanzania anayeamini kuwa naweza, anichangie alicho nacho niionyeshe nchi yangu kuwa mimi si kichaa, bali walikuwa wanazuia maendeleo ya nchi yangu bila kujua. Na wewe utakuwa umejiwekea bima ya maisha kwa kupata mrabaha (royalty) wa asilimia 100 ukiwahi kuchangia hadi tarehe 21/07/2019 na asilimia 20 watakaochangia kuanzia 22/07/2019.

Kwa kweli nitatamani siku moja watu hao wanaokazana kunipeleka Psychiatric wanipe majibu ni kwanini walinifanyia fitina hizo za ovyo ili nionekane kwenye jamii kuwa mimi ni mmoja ya wagonjwa wa akili wakati si kweli, kwa sababu, sababu zote za kunilaza wodi za magonjwa ya akili ni matukio ya kutunga, si yangu.

Hoja yangu hapa; kama yaliyonipata, tukihesabu ni wakati gani wa thamani ambao nilipoteza, wakati ambao ningeutumia kupata maono ya kusaidia maendeleo ya taifa langu kiuchumi na watu wangu.

Naomba Watanzania tubadilike, tupendane, tuache kuoneana wivu na tusaidiane pale unapokuwa nacho, msaidie mwingine mwenye fursa ya maana ainuke, kwa sababu atasaidia wengi. Si lazima eti kila mtu mwenye kuhitaji mtaji aende benki. Ndiyo benki zipo, lakini benki ni taasisi si wakati wote kila mtu mwenye mipango mizuri ya miradi anaweza kupata mkopo, ni hapana.

Ni kinyanyuka tena kiuchumi, natoa ahadi au nadhiri yangu ya kusaidia watu wenye ubunifu makini wa uvumbuzi wa teknolojia na fursa za biashara au miradi kuwasaidia bila masharti, kwa sababu nimejionea mwenyewe isivyo rahisi kupata mitaji kutoka kwa matajiri au taasisi za fedha.

Kama mimi baada ya mradi wa Sabasaba wa mwaka 2016 kufilisika baada ya kuzuiwa matangazo na promosheni siku mbili tu baada ya kumaliza uzinduzi ambao ulinighalimu karibu Sh milioni 850. Kwa hiyo tulijitahidi kurejesha mikopo lakini baadaye, ikabidi taasisi walizotukopesha kuuza mali zetu baada ya kushindwa kulipa.

Kwa hiyo kwa sasa hakuna benki ambayo inaweza kutukopesha fedha hadi tusimame tena kibiashara kwa sababu bado tuna hati chafu ya kurejesha mkopo wa 2016.

Ndipo katika kuzunguka kwangu kwa wafanyabiashara na viongozi wakubwa wa kitaifa wanisaidie mitaji; lakini kila mmoja akawa ananiona mimi mwendawazimu, na cha kushangaza baada ya muda wananikatia mawasiliano (wana ni block), hakika inatia uchungu sana.

Ndiyo maana nimeleta: “MPANGO HUU MAALUMU KWA NGUVU YA UMMA (BUSINESS PROPOSAL TO THE PUBLIC,” ili kila mwenye kidogo au kikubwa na anaona uchungu na nchi yetu na kwa mimi mwana maono ya fursa, anichangie mimi Mtanzania mwenzenu – ili nitumie uwezo huu ambao Mungu amenizawadia uliletee taifa maendeleo pamoja nanyi nyote.

Pia, nanyi mpate asante (royalty) ya maisha kutokana na mchango wako wa hiari kwangu, hii ni asante ambayo natambua hutaipata kokote duniani katika biashara ya kuchangia mitaji au katika biashara ya kukopa na kukopesha.

Kwa hiyo nimebuni mkakati huu maalumu wa kushirikisha ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wenzangu katika kupata mtaji wa kuanzishia miradi hii ambayo ipo tayari, ili iweze kutusaidia na kusaidia jamii; kuliko kutegemea kusubiri mikopo ya taasisi za fedha ambayo ina mlolongo mrefu hasa kwa miradi inayofufuka au inayoanza.

Nikiwa mwana maono (visionary), nilifikiri na kutafakari na hatimaye nikaja na mkakati huu kabambe. Na nikatiwa nguvu kubwa ya kuuanzisha kwa sababu utakupa faida kubwa wewe mchangiaji na ambao utakuwa na faida ya maisha kwa mchangiaji yeyote; tofauti na michango tunayofanya kwa ajili ya harusi, sherehe, michezo na mambo mengine. Kumbe pesa hiyo tunayotupa kwenye starehe, twaweza kujiamini na kuchangia mambo ambayo yanaweza kuleta maendeleo kwa ajili yetu na vizazi vyetu.

Na kwenye barua hii nimetuma link ya makala katika Gazeti la Uhuru la Januari, 2017, iliyokuwa Barua ya Wazi kwa Rais kwamba taifa letu lina watu wenye maono ya uwekezaji bali tunakandamizwa na kurudi nyuma bila sababu. Wakati tungefanikiwa na taifa lingekuwa limefanikiwa.

Ndugu zangu, mambo yote yanawezekana kwa uwezo wake Mungu, hasa Mungu anapotumia watu wake (wana maono) ambao wamo wengi katika jamii zote duniani. Bali tumeshindwa kuwatambua na kuwatumia kwa sababu ya woga, kutojiamini na kuogopa hasara (risk) na wivu usio na faida. Lakini kama nilivyosema hapo juu, hatupaswi kuwa na woga wa kutoa pesa ili kujaribu fursa, bali unatakiwa ujiamini kuwa utapata pesa. Na ikitokea ukakosa wakati wa kujaribu, haupaswi kuvunjika moyo hata kidogo, bali unapaswa kusonga mbele kama hakuna lililotokea.

Kwa sababu pesa tunazotupa kwenye tafrija ni nyingi sana na kamwe hazitarudi. Tofauti na ukichangia miradi au biashara, kuna asilimia 50 kupata faida au asilimia 50 kukosa; lakini hii ikitokea ukapata hasara chukulia ni bahati mbaya (risk); lakini kwa upande wa kujaribu miradi unakuwa umetumia busara na hekima zaidi kuliko tunavyochangia bila shuruti starehe.

Mkiogopa hasara kila wakati ndugu zangu, kamwe hamuwezi kupiga hatua ya maendeleo. Waliobuni ndege wangekuwa  waoga wa kuruka na vyombo walivyobuni, bila shaka leo tusingekuwa kabisa na ndege. Wanaokwenda kwenye sayari za anga ya juu wangekuwa waoga, leo kusingekuwa na wanaokwenda huko.