Kuna tatizo kubwa sana katika suala la hili, wahadhiri wengi katika idara ya Elimu na taaluma za jinsia wanafundisha masomo wasiokuwa na ubobevu nayo.

Mfano:

i. Mhadhiri ana shahada ya uzamili katika uongozi wa elimu, anafundisha historia kwa wanafunzi wa shahada. Eti kwasababu katika elimu yake ya shahada ya kwanza alisoma historia.

ii. Mhadhiri ana shahada ya uzamili ya sanaa katika Elimu, anafundisha Kiswahili.

Ushauri: Ili kutoa wanafunzi bora na wenye weledi katika fani zao lazima mhadhiri atakayefundisha awe hatua moja mbele katika fani hiyo. Hivyo menejimenti ishauriwe, izingatie suala la ubobevu wa fani kwa wahadhiri wake. Kama hakuna wahadhiri wa kutosha katika fani hiyo, watumiwe wahadhiri wa muda, wakati chuo kikijipanga kuondoa changamoto hiyo.

 

c. Wanafunzi Kufaulishwa

Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wahadhiri kuwa wanalazimishwa kufaulisha wanafunzi, na wasipofanya hivyo hutishiwa. Hii imesababisha kuzalisha wanafunzi wasiokuwa na ubora. Japo suala hili halina ushahidi wa kutosha, lakini ushahidi wa kimazingira unaonesha ni kweli. Kwamba aina ya wanafunzi wanaomaliza kozi mbalimbali hususan Cheti na Stashahada.

Pia waweza kupitia aina ya maswali yanayotungwa kwa ajili ya wanafunzi, na vitabu vya majibu (scripts) kwa kutumia sampuli tete.

 2. MAPENDEKEZO YA TAARIFA MBALIMBALI

a. Uongozi uliopita ulitolewa na kuletwa uongozi mpya kwasababu ya tuhuma mbalimbali. Naomba uombe ripoti ya tume iliyoundwa na NACTE. Miongoni mwa masuala yaliyoongolewa ni:

(i) Kuchukuliwa hatua dhidi ya watumishi waliochakachua matokeo

(ii) Kuchukua hatua dhidi ya ajira mbili za mtumishi Rodgries Kiowi

 

b. Ripoti ya PPRA dhidi ya taarifa 2013/2014 dhidi ya ujenzi wa jengo la hosteli (hii ninayo ukihitaji) inaeleza juu ya ujenzi wa kiwango cha chini cha jengo la hostel na hatua zilitakiwa kuchukuliwa dhidi ya wahusika lakini hazikuchukuliwa.

 

3. UDHAIFU WA MENEJIMENTI

a. Mahusiano Mabaya Kati ya Menejimenti Timu

Menejimenti yaani Mkuu wa chuo, Naibu Mkuu wa chuo Taaluma na Naibu Mkuu wa Chuo Utawala, Mipango na Fedha hawana mahusiano mazuri hata kidogo. Kila mmoja amekuwa akimlaumu mwenzake. Kuthibitisha hili waweza kuwahoji wote ukianzia na wa nchini, kwani kila mfanyakazi sasa anajua suala hili.

  

b. Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma Kutofanya Kazi za Taasisi

Naibu Mkuu wa Chuo amekuwa hafanyi kazi zake, bali majukumu yake yote amekuwa akiyakasimisha kwa wakuu wa idara kwa muda wa miezi sita sasa (6). Hivyo kufanya masuala mengi ya kitaaluma kutopiga hatua. Ushahidi wa suala hili upo wazi aulizwe aoneshe kazi alizofanya ndani ya mwizi mmoja tu au wiki atakayoulizwa, amefanya nini.

Amekuwa akifanya haya ili kumkomoa Mkuu wa Chuo ambaye alimzuia matumizi mabaya gari la taasisi pia matumizi mabaya ya ofisi, kwa kuwa na mahusiano tata na Katibu Muhtasi wake.

 

c. Madai ya Wafanyakazi

Wafanyakazi Wanataaluma na waendeshaji wanakidai chuo zaidi ya milioni mia nne (400). Madai haya yanazidi kuongezeka kwani hakuna jitihada zinazochukuliwa kupunguza madeni haya.

 

Madeni haya yanatokana na:

 i. Posho kwa ajili ya Nauli sh 20,000

 ii. Posho za nyumba 5% ya mshahara

 iii. Posho za Usimamizi wa mitihani

 iv. Posho za Usahihishaji wa mitihani

 v. Posho za Usimamizi wa tafiti za wanafunzi

 vi. Posho za Malipo ya kazi za ziada kwa waendeshaji

 vii. Posho za vikao

 

Kutolipwa kwa madai haya imesababisha wafanyakazi kuuchukia uongozi wa chuo hivyo kufanya kazi pasi ari.

 

Pamoja na madeni haya chuo kina madeni makubwa ya nje zaidi ya sh milioni mia nane (800).

 Ushauri: kwa kuwa Chuo kwa sasa hakina mapato ya kutosha menejimenti iwaeleze ukweli wafanyakazi kuwa mapatao ya chuo hayawezi kulipa baadhi ya masuala, hivyo isitishe malipo hayo. Lakini ilipe malipo yote ambayo inadaiwa kabla ya kusitisha. Hii inatokana na kwamba mapato yapatikanayo ndani ya taasisi hayakidhi mahitaji. Taasisi iyarudishe malipo hayo kama motisha mara hali ya kifedha ikiwa nzuri, ama italeteleza kukua kwa deni na pia amani kutoweka mahala pa kazi.

 

d. Baraza la Wafanyakazi

Tokea menejimenti hii iingie madarakani, hakuna baraza la wafanyakazi, hivyo kusababisha manung’uniko mengi kutoka kwa wafanyakazi. Endapo baraza hili lingekuwepo lingepunguza malalamiko kwa kiasi kikubwa.

 

e. Matumizi mabaya ya madaraka ya mkuu wa chuo

i. Mkuu wa chuo alitumia vibaya madaraka yake na kwa maslahi binafsi kwa kuajiri watu kinyume cha taratibu, wakati akijua kanuni na taratibu. Ajira za kuhamisha watumishi ziliratibiwa na ofisi yake kwa kutumia makatibu muhtasi na afisa mahusiano. Suala hili litailetea serikali hasara kubwa.

ii. Ajira za watu watano (5) nazo ni matumizi mabaya ya madaraka kwani watu hao hawakuombewa kibali kutoka utumishi.

iii. Ukiukwaji wa manunuzi. Kuna ukiukwaji mkubwa wa manunuzi.

i. Mfano kuna mashine ya kuchuja maji chumvi, Mkuu wa chuo alimleta mtu anayemfahamu yeye peke yake akakiuzia chuo mashine. Lakini baada ya wiki mbili mashine ile iliharibika. Mpaka leo ile kampuni haijulikani hata ofisi yake, chuo kimeingia hasara ya shilingi milioni kumi na mbili.

ii. Upakwaji wa rangi jengo la Uhuru, Mkuu wa chuo alimleta fundi anayemjua yeye pasi kutangaza tenda

iii. Mkuu wa Chuo ameleta maombi ya mzabuni mmoja tu, kwa ajili ya kuweka viti jengo la Zanzibar na kulazimisha kamati ya tenda impe mzabuni huyo tenda ya sh 560 milioni.

 

4. UDHAIFU WA BODI

Bodi mpaka sasa haijakamilika kwani kulingana na kanuni kuna wajumbe wamelimaliza muda wao na hawajateuliwa, yawezekana kabisa suala hili limeleteleza bodi kutofuatilia masuala mbalimbali. Mpaka sasa kuna wajumbe 6 kati 11 ya wajumbe wote.

 Tokea mwaka 2013 Septemba Bodi ya Chuo haina Mwenyekiti, hili pia linawezekana ikawa ni tatizo kwa bodi ya chuo.

Pia Uwepo wa Mkurugenzi Ufundi ndani ya Bodi inasababisha ashindwe kuwajibika, kwa sababu yeye ni sehemu ya tatizo. Wakati yeye alipaswa asimamie taasis ipasavyo.

 

5.   UDHAIFU WA WAFANYAKAZI

Wafanyakazi wengi hawafanyi kazi ipasavyo, wamekifanya Chuo kuwa kijiwe cha kupita, hawafanyi kazi za chuo kwani muda mwingi hawapo kazini.

Kazi za mwanataaluma ni 3, kufundisha, kutoa ushauri wa kitaalamu na kufanya tafiti. Mpaka sasa hakuna mhadhiri ambaye anatoa ushauri wa kitaaluma na hata kufanya tafiti tokea uongozi huu uingie, huu ni udhaifu wa wahadhiri.