Kundi la watu wazee kutoka Korea Kusini kwa sasa wako nchini Korea Kaskazini kukutana na jamaa zao wenye hawajawaona tangu vimalizike vita vya mwaka 1950-1953.
Vita hivyo vilisababisha rasi ya Korea kutengana na watu waliokuwa wanaishi upande wa Kaskazini wasikuwe na uwezo wa kuondoka.
Korea hizo mbili ambazo bado ziko kwenye mzozo wa vita, zilikuwa zimepanga shughuli ya kuwakutanisha watu hao awali lakini shughuli hii ndiyo ya kwanza kwa miaka mitatu.
Watu kutoka nchini Korea walichaguliwa mwa mfumo wa bahati nasibu huku mtu mzee zaidi katia kundi hilo akiwa wa umri wa miaka 101.
Mikutano hiyo mifupi huenda ndiyo ya mwisho wengi wataonana.
Ni kina nani wanadhudhuria?
Kuna raia 83 wa Korea Kaskania na 89 wa Korea Kusini wanaoishukia katika shughuli hiyo ya kukutana.
Watu 100 walikuwa wamechaguliwa kutoka kila upande lakini wengine waliondoka baada ya kufahamu kuwa jamaa zao waliokuwa na matumaini ya kuwaona hakuwa hai tena.
Mwanamke mmoja mweny miaka 92 aliwaambia waandishi wa habari kuwa alikuwa anaenda kumuona mtoto wake wa kiume kwa mara ya kwanza tangu vita vimalizike.
Lee Keum-seom alisema alitengana na mtoto wake ambaye wakati huo alikuwa mweye umri wa miaka minne na pia mume wake alipojaribu kutoroka.
“Sikutarajia kuwa siku hii ingekuja, aliliambia shirika la AFP. Sikujua hata kuwa alikuwa bado hai au la.
“Nina zaidi ya miaka 90 kwa hivyo sijui nitakufa lini,” Moon Hyun-sook aliliambia shirika la Reuters. Alikuwa anasafiri kwenda kukutana na dada yake mdogo.
“Ninashukran nyingi sana kwamba nimechaguliwa wakati huu, nina furaha sana.”
Kwa nini mkutano huu ni muhimu?
Kwa muda wa miaka mitatu, na wakati kumekuwepo na utulivu, Korea hizi mbili zimepanga makundi ya watu kutembeleana. Kumekuwa na shughuli 20 kama hizo kwa kipindi cha miaka 18.
Mikutano ya awali kati ya kaka na dada, wazazi na watoto na waume na wake zao imekuwa yenye hisia nyingi.
Lakini kutokana na sababu kuwa wale waliotenganishwa wanazidi kuzeeka, muda unazidi kwisha.
Watu hawa wanakutana vipi?
Raia wa Korea Kusini wanasafiri kwa basi kupitia kwa mpaka wenye ulinzi mkali kwenda eneo moja la kitalii kwenye mlima Kumgang.
Watakaa upande huo wa Korea Kaskazini kwa siku tatu lakini watapewa muda wa saa chache kukutana na jamaa zao kila siku kwa jumla saa 11. Mikutano yao mingi itafuatilia kwa karibu sana.
Wengi wanaleta zawadi kama nguo, madawa na chakula kwa jamaa zao kwenye taifa mskini la Korea Kaskazini.
Haki miliki ya picha EPA Image caption