Korea Kaskazini imezindua kombora jipya la masafa marefu ambalo ukubwa wake umeshangaza hata wachambuzi wa masuala ya silaha ya nchi hiyo. Mtaalam wa masuala ya ulinzi Melissa Hanham anaelezea kombora hilo ni nini na kwanini ni tishio kwa Marekani na ulimwengu.

Katika kuadhimisha miaka 75 ya chama tawala cha Workers Party nchi hiyo imefanya gwaride la kijeshi wakati wa usiku wa Jumamosi.

Hafla hiyo iliyoangaziwa sana ilionesha fahari yake na hali zote ambazo ulimwengu umetarajia kutoka kwa maonesho ya watu wa Korea Kaskazini.

Pia tukio hilo liliandamana na hotuba yenye hisia kutoka kwa mwenyekiti wa chama hicho Kim Jong-un , ambaye kuna wakati alidondosha machozi akielezea magumu ambayo Korea Kaskazini imeyapitia. Si hayo tu, ilionesha kombora la masafa marefu (ICBM)

Hili ni kombora la namna gani?

Haya ni mambo matatu tunayoyafahamu kuhusu kombora hili. Ahadi ya Kim ya silaha ya kimkakati tarehe 01 mwezi Januari , Bwana Kim alitoa hotuba yake ya mwaka mpya ambapo alitangaza kuwa Korea Kaskazini ”inatengeneza mfumo wa kisasa wa silaha ambazo humilikiwa na nchi zilizoendelea pekee”.

Hususani alielezea kama zoezi la ”kimkakati” akimaanisha mfumo wa silaha za nyukilia .

Bwana Kim akiigusia Marekani, alisema “katika siku za usoni, kadiri Marekani inavyokaa kwa muda na kusita katika usuluhishi wa uhusiano wa DPRK na Marekani ndivyo itakavyoshindwa zaidi mbele ya nguvu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea, ambayo inaendelea kuimarika na nguvu zaidi ya ilivyotabiriwa.

ICBM mpya ni silaha ya mkakati iliyoahidiwa na Bwana Kim. Inalenga Marekani kabisa, na imekuwa kama jambo lililofanyiwa maamuzi mbele ya mazungumzo yaliyoshindwa na serikali ya Trump.

Tishio jipya la mifumo ya kujilinda na makombora Marekani
Korea kaskazini amefanyia majaribio makombora mawili ya masafa marefu ICBM . Kombora la Hwasong – 14 lilijaribiwa mara mbili 2017 na huku likiwa linaweza kushambulia umbali wa 10,000km (6,213 maili) linaweza kufika kushambulia eneo lolote la Ulaya magharibi na takriban nusu ya eneo la bara la Marekani likiwa limebeba kichwa kimoja cha kinyuklia.

Kombora jipya la ICBM ambalo bad halijafanyiwa majaribio, pia ni kombora la awamu mbili lakini lina nguvu na ni pana zaidi ya kombora la Hwasong-15. Hadi pale mashine yake itakapofichuliwa ama hata kufanyiwa majaribio sio rahisi kubaini linaweza kuruka umbali gani.

Badala yake wanaangazia kuhusu kujaribu kuzindua urushaji wa vichwa vitatu vya kinyuklia katika kombora moja .

Hili litakua pigo jingine kwa mifumo ya kujilinda na makombora ya Marekani kutokana na kila kichwa cha kinyuklia , ikimaanisha kwamba italazimisha mifumo hiyo kurusha makombora matatu kwa mpigo kudungua makombora hayo.

Mataifa yalio na silaha za kinyuklia yana mifumo inayoweza kudungua kombora la kinyuklia lenye vichwa vitatu na sasa Korea Kaskazini nayo ipo katika mipango kama hiyo

Ni suala linalozua wasiwasi mkubwa
Kuna maswali mengi ya mintindo inayosalia kujibiwa kuhusu kombora la ICBM lenyewe , kihusu ni lini litafanyiwa majaribio ama hata kupelekwa. Hatahivyo gari linalobeba kombora hilo ndio linalotia wasiwasi.

Mojawapo ya vizuizi vikubwa vya uwezo wa Korea Kaskazini kushiriki katika vita vya nyuklia ni idadi ya mashine za kurusha makombora hayo.

Ukweli ni kwamba unaweza kurusha makombora Marekani inakadiria kwamba Korea Kaskazini inaweza kurusha makombora 12 ya ICBM pekee.

Hesabu hiyo inatokana na nadharia kwamba kila moja ya mashine sita za kurusha makombora hayo inaweza kurusha kombora moja la ICBM na kung’ang’ania kurusha kombora la pili kila moja kabla ya Marekani haijajibu.

Mwaka 2010, Korea Kaskazini ilinunua magari matano makubwa kutoka China na kuyabadilisha kuwa na uwezo wa kurusha makombora TELs.

Ni magari hayo ya TELs ambayo Korea Kaskazini iliyatumia katika onesho lake la gwaride , kubebea na kusimamisha makombora hayo ya ICBM.

Magari hayo ni mazuri hali ya kwamba yanaweza kuyaondosha makombora hayo kabla ya kurushwa, kwasababu ni vigumu kuchukua mahala pake iwapo kombora hilo litashindwa kuruka.

Gwaride hilo linaonesha kwa mara ya kwanza magari matano. Mahari hayo matano yalibadilishwa.
Ni wazi kwamba Korea Kaskazini ina uwezo wa kupata vifaa vya kutengeneza mashine za kurusha makombora makubwa licha ya vikwazo na udhibiti wa kuuza bidhaa zake nje ya nchi.

Pia ni wazi kwamba wameunda sekta yake ya viwanda kuweza kufanyia mabadiliko mbali na kuzalisha mitambo yake ya kurusha makombora.