Serikali imeamua kuanzisha mfumo  wa uotoaji risti kwa kutumia Mashine za Kielekitroniki za Bodi (EFD). Kwa mujibu wavuti ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mfumo huo  unachukuwa nafasi ya mashine za rejesta za fedha ambazo zimekuwa zikitumika zamani.

Mashine hizo hazikukidhi mahitaji yaliyotarajiwa ikiwa ni pamoja na kurahisisha mauzo kwenye sehemu za biashara.

Mfumo huo mpya umeanzishwa ili kuondoa udhaifu wa mfumo wa zamani na pia kuhakikisha kwamba unarahisisha usimamizi wa kodi na kukidhi matarajio ya ukusanyaji wa mapato ya serikali.

Madhumuni

Uanzishaji wa mfumo mpya wa utoaji wa risti za kodi za kielekitroniki kwa lengo la kurahisisha usimamizi wa kodi na kudhibiti mauzo kwa watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania pamoja na wadau wengine.

Mfumo huu ulianza rasimu Julai 1, 2010 kwa wafanyabiashara waliosajiliwa na VAT wafanyabiashara hawa hawatumii tena rejesta za fedha wala risti za ankra zilizoandaliwa na kwa mkono isipokuwa mashine.

Mfumo wa kodi wa kielekitroniki nini

Mfumo wa kutoa risti wakielektroniki kwa kutumia mashine za kielekitroniki.

Mfumo unaleta ufanisi katika kuweka kumbukumbu za mauzo na uthibiti wa bidhaa mashine hizo.

 

Pia zinarahisisha usimamizi wa kodi kwa gharama nafuu na matumizi yake yanahamasisha ulipaji wa kodi kwa hiari.

Wamiliki wa mashine hizo wanatakiwa kutunza kumbukumbu za mauzo ya kila siku ambazo zitakuwa zikionekana moja kwa moja TRA kwa njia ya mtandao.

Mashine hizo zina uwezo wa kuhakikisha urahisi wa utoaji wa taarifa na kutoa ishara pale ambapo hujuma katika mashine itatokea.

Pia zitatoa taarifa zote muhimu zitakazotumika katika usimamizi wa udhibiti wa kodi.

Aina za mashine za kielekroniki

Mashine za EFD ambazo zitatumika Tanzania Bara ni za aina tatu rejesta ya kodi za kielekitroniki. Rejesta hii hutumika kwa wafanyabiashara wa rejareja ambao wanatoa risti kwa wa maandishi ya mkono na wale wote ambao watakuwa wanauza bidhaa kwa kutembeza kwa wateja.

Printa ya kodi za kielekitroniki

Mashine hii hutumiwa na wafanyabishara wa rejareja ambao wanatumia kompyuta katika utoaji wa risti na nakara na madai. Mfano wa mashine hizo hutumika katika maduka makubwa ya rejareja vituo vya mafuta na shughuli za ukataji wa risti.

Mashine za alama za kieletroniki za kodi

Mashine hizo hutumika kwa wafanyabiashara ambao hutumia program maalumu za uhasibu katika utoaji wa risti na ankra za madai.

 

Mashine hizi zina uwezo wa kutambua ankra na risti zote zinazotolewa na kompyuta zinazohusu mauzo.

 

Nyaraka nyingine zote zitolewazo ambazo hazihusu na mauzo hazitatiwa alama na mashine hiyo.

 

Mashine hizo hutumiwa na wafanyabiashara na wazalishaji wa jumla.

Ni jukumu la kila mfanyabiashara kuchagua na kutumia mashine inayofaa kulingana na biashara yake.

Mashine zina ubora wa aina gani

Mashine za kielekitroniki zina ubora ufuatao: Kumbukumbu katika kitufe chake haziwezi kuharibika na kemikali ya aina yoyote wala muingiliano wa sumaku.

Mashine zitatoa taarifa ya mauzo ya siku kila baada ya sasa 24.

Mashine zitatuma taarifa za kodi moja kwa moja TRA haziruhusu kubadili tarehe.

Zitatoa risti ambazo ni ngumu kugushiwa.

Zitumika popote pale nchini na kuunganishwa na mtandao wa TRA.

Zina uwezo wa kufanya kazi kwa saa 48 umeme unapokosekana na zinaweza kutumia betri.

Kumbukumbu hutunzwa bila kufutika pindi tu zinapoingizwa, zina uwezo wakutunza kumbukumbu kwa miaka mitano.

Vigezo vya mashine ya kodi ya kielekitroniki

Kuna namba ya siri ambayo mmiliki ataitumia wakati wa kuanza kutumia mashine na vilevile kuwa na uwezo wa kubadili namba hiyo inapobidi.


Uwezo wa kudhibiti kumbukumbu kutoharibiwa. Uwezo wakujua usahihi wa taarifa. Uwezo wa kuzuia vitendo visvyo sahihi kufanyika.


Uwezo wa kufanya marekebisho bila kuharibu mfumo wa usalama wa mashine.


Uwezo kuchukua taarifa na kuzitunza bila taarifa hizo kuharibiwa kwa namna yoyote. Uwezo wa kuhifadhi umeme kwa saa 48 baada ya umeme kukatika.


Uwezo wa kutoa ripoti kabla ya mabadiliko yoyote kufanyika katika mashine.

Nani mtumiaji wa mashine hizo za kielekitroniki

Watumiaji wa mashine hizo ni wafanyabiashara wote wenye viwanda biashara ya jumla rejareja ambao wamesajiliwa na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na wale ambao wanatambuliwa na kamishina kutumia mashine hizo.

Wajibu na haki za mtumiaji wa mashine ni zipi

Matumiaji wa mashine atakuwa na wajibu wa haki zifuatazo watumiaji wana haki ya kununua mashine hizo kutoka kwa msambazaji yeyote aliyethibitishwa na TRA.

Mwenye mashine hizo wataunganishwa kwenye mfumo wa mawasiliano wa TRA na pia wana wajibu wa kuhakikisha kwamba mauzo yote kibiashara yanaongia kwenye mfumo huo.


Watumiaji wanatakiwa kutoa risti kwa wateja kutoka kwenye mashine.

Watumiaji wanatakiwa kutenda haki na kutunza mashine kama ilivyoanishwa na watengenezaji

 

Watumiaji  wanatakiwa kutoa taarifa kwa maandishi kwa wasambazaji na kwa kamishna au Meneja wa Mkoa wa TRA  ndani ya saa 24 pale ambapo mashine zitaharibika.


Ikitokea mtumiaji wa mashine ameweka taarifa zisizo sahihi kwenye mashine kimakosa anaweza kuendelea na biashara bali anatakiwa kutunza kumbukumbu za mkosa hayo kwa ajili ya ufuatiliaji utakaofanywa na wakaguzi.


Marekebisho yote katika mashine yatafanywa kwa misingi iliyoanishwa katika taratibu ndani ya sheria ya VAT na kanuni zake.


Wamiliki wa namna yoyote hawatakiwi kuhamisha mashine hizo kwenda kwa matumizi ya mtu mwingine.


Wamiliki wana wajibu wa kuhakikisha mashine hizo zinawekwa mahali ambapo ni rahisi kwa wateja kupata huduma.