Leo tarehe 21 Aprili 2025, dunia imepata pigo kubwa kufuatia taarifa rasmi ya kifo cha Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis.

Vatican imethibitisha kuwa Papa Francis amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88, baada ya kusumbuliwa na matatizo ya kiafya kwa muda mrefu.

Papa Francis, ambaye jina lake halisi ni Jorge Mario Bergoglio, alizaliwa Argentina na kuwa Papa wa kwanza kutoka Amerika ya Kusini mwaka 2013.

Alifahamika kwa moyo wake wa upendo, huruma, na kusimama na wanyonge. Uongozi wake uliweka historia kwa kusisitiza mshikamano, haki za binadamu, na utunzaji wa mazingira.

Dunia nzima inaomboleza kifo cha kiongozi huyu mwenye busara na hekima. Mungu ailaze roho ya Papa Francis mahali pema peponi.