Na Magrethy Katengu,JamhuriMedia, Dar es Salaam

Chama cha National League for Demokracy (NLD) Kimemuidhinisha Doyo Hassan Doyo kuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama.hicho katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025 huku Mfaume Khamisi Hassani akiidhinishwa kiwania Urais wa Zanzibari

Akizungumza mara baada ya Uchaguzi huo Aprili 10, 2025 amesema Chama hiko wanapenda Taifa la Tanzania na hawapo tayari kujihusisha na chama chochote kutoshiriki Uchaguzi hivyo watashiriki zoezi hilo mpaka mwisho na. wanalinda tunu ya Amani iliyopo.

” Chama cha NLD tutaweka wagombea Nchi nzima hatuko tayari kususia Uchaguzi wala kuleta sababu zisizo kuwa na mashiko tuna Imani Sera zetu zitawafikia watanzania watatuchagua “amesema Doyo

Hata hivyo ameshukuru Chama chake kumuamini kuipeperusha kwa.kumpa dhamana ya kuwania Urais hivyo anaaihidi Watanzania wakimchagua atapambana na Mafisadi wala rushwa wote kwa kuweka adhabu ya viboko 24 kwa yeyeyote atakayebainika katika Serikali yake

Naye Mgombea Urais Zanzibar Mfaume Khamisi Hassani ameshukuru kwa chama hiko kumuamini kwenda kupeperusha bendera ya NLD atahakikisha Wazanzibari wakimpatia Kura Serikali itakayoundwa itashughulika kutatua kero za wananchi zote zilizokuwa zikiwakabili .

Awali Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Sisty Nyahoza ambaye lihudhuria kushuhudia Uchaguzi huo wa NLD amesisitiza kuwa chama chochote kilichosajiliwa kikatiba kinatakiwa kushiriki Uchaguzi hivyo amefurahishwa na mwenendo wa chama hiko.