Baada ya kutangaza nia ya kugombea Urais, hatimaye Dorothy Semu amechukua fomu ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Fomu hiyo amekabidhiwa na Katibu wa Mipango na Uchaguzi Taifa Ndugu, Shaweji Mketo katika Ofisi za Makao Makuu ya @ACT Wazalendo Magomeni, Dar Es Salaam.

Mara baada ya kukabidhiwa fomu, Ndugu Dorothy Semu akasema, “leo nimechukua fomu ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na niko tayari kumkabili Rais Samia Suluhu Hassan na chama chake CCM—chama ambacho kimeshindwa kutimiza wajibu wake wa msingi wa kuongoza na kuwahudumia Watanzania.”