Shirika la Umoja wa Mataifa la Wahamiaji (IOM), limeomba msaada wa dola milioni 18.5 kwa ajili ya kutoa huduma za afya kwa watu walioathiriwa na mripuko wa homa ya Mpox Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Mkurugenzi Mkuu wa IOM, Amy Pope amesema kusambaa kwa virusi vya Mpox katika eneo la Mashariki na Kusini mwa Afrika, ni jambo linaloleta wasiwasi mkubwa.

Pope amesema wasiwasi mkubwa umeonekana kuwepo kwa wahamiaji wanaoishi katika mazingira magumu, watu wanaohama sana na jamii zilizohamishwa ambazo mara nyingi hazizingatiwi katika majanga.

Wakati huo huo,Thailand imegundua uwepo wa mgonjwa mmoja ambaye anadaiwa  kutokea  Afrika akiwa na homa ya Mpox.

Hatahivyo Idara ya Kudhibiti Magonjwa imesema inasubiria majibu ya vipimo ili kuweza  kubaini kama ni aina mpya ya kirusi cha homa ya Mpox  Clade 1b.