Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Waziri wa Katiba na Sheria Dk Damas Ndumbaro ameziagiza Bodi mbalimbali za Wadhamini wa taasisi ambazo zimemaliza muda wake wa uongozi kufanya uchaguzi mara moja ndani ya kipindi cha miezi miwili.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa semina maalum iliyoandaliwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kwa ajili ya wajumbe wa Bodi za Wadhamini wa Taasisi zilizopo kwenye mkoa wa Dar es Salaam iliyokuwa na kauli mbiu “Uwajibikaji wa Bodi za Wadhamini kwa Ulinzi wa Mali za Taasisi na Maendeleo ya Jamii”, Dkt Ndumbaro alisema kuwa bodi hizo ni lazima kufanya uchaguzi ndani ya kipindi hicho ili kupata viongozi halali.
“Naziagiza bodi zote za wadhamini za taasisi mbalimbali ambazo muda wao wa uongozi umekwisha wafanye uchaguzi mara moja kwani siku zimeisha,” alisema Dkt Ndumbaro.
Dkt Ndumbaro pia waliwataka viongozi wa bodi za wadhamini ambao muda wao umekwisha wasing’ang’anie madaraka na kusababisha migogoro isiyo na ulazima.
Pia amezitaka bodi hizo kufanya kazi kwa umoja na ushirikiano kwa maendeleo ya taasisi wanazoziongoza.

“Nawasihi tena viongozi wa bodi za wadhamini kudumisha amani na umoja kwenye taasisi zenu, kwani migogoro hiyo msipoizuia inaweza kuleta madhara makubwa kwenye taasisi zenu na kwa taifa kwa ujumla” alisema Ndumbaro.
Aidha, Dk Ndumbaro aliwataka wadhamini wa bodi kutumia 4R’s za Rais Samia Suluhu Hassani ili ziweze kuleta muafaka kwenye taasisi zao badala ya kuendeleza migogoro ambayo haina afya na kuzorotesha taasisi hizo.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Usajili, ufilisi na Udhamini (RITA), Dkt Amina Msengwa alisema semina hiyo ilijielekeza kutoa elimu kwa viongozi wa bodi hizo na kuwakumbusha majukumu yao wakiwa kama wasimamizi mali za taasisi husika.
“Kitu ambacho tumegundua ni kwamba, wadhamini wengi wanadhani kuwa wao ni wamiliki wa mali hizo na kuzitumia mali za taasisi hizo kwa manufaa yao binafsi” alisisitiza Dkt Msengwa.
Dkt Msengwa aliongeza kuwa wanaamini semina hiyo itasaidia kuwakumbuka viongozi wa bodi hizo majukumu yao ya kisheria .
Kwa upande wake Kabidhi Wasihi Mkuu na Mtendaji Mkuu wa RITA, Bw. Frank Kanyusi alisema kuwa semina hiyo ililenga kupunguza migogoro katika taasisi hizo ambazo baadho yao zimekuwa katika migogoro ya mara kwa mara.
“Tumeamua tufanye semina hii hapa Dar es Salaam kwa sababu mkoa wa Dar es Salaam ina bodi za wadhamini zaidi ya asilimia 65, hivyo elimu hii ilihitajika sana hapa kuliko maeneo mengine”, alibainisha Bw Kanyusi.
Hata hivyo Bw. Kanyusi alisema kuwa wana mpango wa kuendelea na semina hizo katika mikoa mbalimbali ya hapa nchi kwa lengo la kuendelea kuongeza uelewa kwa mabaraza ya wadhamini mbalimbali nchini na kukumbusha majukumu yao.
Mmoja wa bodi ya wadhamini kutoka katika kanisa la TAGT Airport Dar es Salaam Mchungaji Godwin Chimaisi alisema kuwa semina waliyoipata itawasaidia na kuwakumbusha majujumu yao ya kila siku.
“Semian hii imeongeza uelewa wetu juu ya majukumu ya wadhamini na kutukumbusha kwani kuna kipindi huwa tunajisahau na kufanya tofauti na vile ambavyo inatakiwa” alisema Mch Chimaisi.
Mchungaji Chimaisi aliipongeza RITA kwa kutoa semina hiyo kwa wadhamini wa bodi mbalimbali kwa sababu itasaidia kuokoa taasisi nyingi ambazo zinakumbwa na changamoto za sintofahamu kuhusiana na mali za taasisi.
“kuna bodi mbalimbali za wadhamini huwa zinafanya mambo zenyewe bila hata kushirikisha wanachama wake, kitu ambacho sio sahihi, hivyo semina hii ni muhimu kwa viongozi wote wa bodi za wadhamini na wanachama wa taasisi mbalimbali. Alisema Mch Chimaisi.
Mjumbe wa bodi ya wadhamini kutoka kwenye taasisi ya Mfuko wa Wadhamini wa Wanawake (WFTT) Bi Nasim Losai, aliipongeza RITA kwa kuandaa semina hiyo na kugusia kuwa uwepo kwa wanasheria umeongeza uelewa wao kwani wadhamini wengi walikuwa hawafahamu masuala ya kisheria kuhusiana na nafasi yao kama wadhamini wa taasisi hizo.
Semina hiyo ilihudhuriwa na washiriki kutoka katika wilaya zote za jiji la Dar es Salaam na washiriki wengine k