Na WMJJWM, CHINA

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu ameshiriki Kongamano la kimataifa la Ushirikiano kati ya China na Africa katika masuala ya Usawa wa kijinsia  (China – Africa Women’s Forum) Tarehe 29 Juni hadi Julai 1, 2023.

Kongamano hilo lililoandaliwa na ‘All China Women Forum’ na kufanyika Jijini Changsha, Jimbo la Hunan nchini China lilikuwa na lengo la kuainisha fursa zilizopo China na Africa kwa ajili ya kuwawezesha wanawake hususan katika nyanja ya uvumbuzi na ujasiriamali.

Sambamba na kongamano hilo, lililokuwa na Kaulimbiu isemayo “Pooling the strength of Chinese and African women, and jointly promoting comprehensive development”, yalifanyika pia makongamano mengine madogo likiwemo kongamano la kilimo lenye lengo la kukuza na kuongeza mnyororo wa thamani kwa mazao ya  Wakulima kwa ushirikiano wa China na Afrika.

Mpango huo utasaidia kuongeza kipato kwa ngazi ya kaya, hali itakayosaidia kupunguza masuala ya ukatili yatokanayo na kipato duni.