Na Dotto Kwilasa,JamhuriMedia,Dodoma

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya Wazazi kinachotarajiwa kufanyika Julai 13 mwaka huu Wilayani Mpanda Mkoani Rukwa.

Hayo yameelezwa leo Julai 24,2024 Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Fadhil Maganya wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma na kueleza kuwa ufunguzi wa maadhimisho hayo Julai 8, mwaka huu katika Mkoa wa Katavi Wilaya ya Mlele kata ya Inyonga kwenye viwanja vya Shule ya msingi Inyonga.

Pamoja na mengine wiki hiyo itatumika kupanda miti zaidi ya 100,000 lengo likiwa ni kutunza na kuhifadhi mazingira kwa kizazi cha sasa na vijavyo.

“Tutakuwa na matukio mengi ikiwemo la Julai 10 ambapo tutakuwa na Baraza kuu la kawaida la Umoja wa Wazazi Tanzania,Julai 11, Julai Kongamano la maadili na Malezi,na Julai 12 itakuwa maalum kwa ajili ya michezo na kauli mbiu ya Sherehe hizo kwa mwaka 2024 ni Uchaguzi 2024/2025, Jumuiya ya Wazazi iko mstari wa mbele, “amefafanua.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ametumia nafasi hiyo kuzungumzia Sakata la Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es laam, Hassan Bomboko kutakiwa kuwalipa Mabilion ya Fedha Madada poa 36 waliokamatwa hivi karibuni kwa madai ya kujihusisha na Biashara ya kuuza miili yao.

Amesema wao kama Jumuiya ya Wazazi ya CCM, wanaungana naye kwa kitendo hicho kwani yeye ndiye msimamizi wa Sheria na Maadili katika wilaya anayoiongoza.

Hatua hii imekuja kufuatia hivi karibuni vyombo vya habari kuripoti kuhusu Sakata la ukamataji wanawake 36, wanaodaiwa kujihusisha na biashara ya ukahaba ambapo taarifa ilisema limechukua sura mpya, baada ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo (DC), Hassan Bomboko kupewa notisi ya kuwalipa Sh36 bilioni Mdada poa hao.

Notisi hiyo ya siku 14 inayoanza kuhesabika Alhamisi, Juni 20, 2024, ambayo inalenga kuwalipa watuhumiwa hao 36 wanaodai wamedhalilishwa kwa kuwaita ‘Dada Poa’ na kuwaweka rumande kwa zaidi ya siku tano kinyume na sheria.

Kulingana na hayo Mwenyekiti huyo amesema Jumuiya ya Wazazi ambayo inasimamia maadili kwenye Jamii inamuunga mkoano moja kwa moja Dc wa Ubungo ambaye aliendesha oparesheni ya kuwakamata wanawake hao wanaodhaniwa kuwa madada poa ambao walikutwa katika mazingira ya kuuza miili yao.

“Jumuiya hii tunamuunga mkono DC Hassani kwa Opareshini ile kwani yeye ndiye msimamizi wa sheria katika wilaya yake na alipowakamata hakwenda kama Hassan bali alienda kama kiongozi serikali anapaswa kuhakikisha kunakuwa na maadili katika eneo lake”,amesema na kuongea;

Tupo pamoja na DC,tunampongeza kwa kazi nzuri aliyo na anayoendelea kuifanya na hapa nitoe wito kwa viongozi wengine katika maeneo yao kuendelea kafanya kazi ya kusimamia sheria na kuhakikisha maadili yanazingatiwa”, amesema