Mgombea nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile akijinadi mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 74 wa WHO leo Agosti 27, 2024 unaofanyika katika Jiji la Brazzaville nchini Congo.

Dkt. Ndugulile amesema vipaumbele vyake katika kazi hiyo endapo atachaguliwa kuwa ni kuhakikisha Watu wanapata haki ya kupata huduma bora za afya; Kuboresha utayari wa nchi za Afrika katika kukabiliana na majanga ya magonjwa ya mlipuko, Kuimarisha uwajibikaji ndani ya WHO kanda ya Afrika pamoja kuimarisha mawasiliano baina ya nchi wanachama katika masuala ya Afya.

Zoezi la uchaguzi wa Mkurugenzi Mkuu wa WHO Kanda ya Afrika unafanyika leo kupitia Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Afya Afrika chini ya Shirika la Afya Duniani.    

Please follow and like us:
Pin Share