Na Mwandishi Wetu, JakhuriMedia, Bagamoyo

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro amesema amepokea ombi la kuongeza siku za kufanyika Tamasha kutoka Nne mwaka huu na kuwa siku Saba kwa mwaka 2025.

Dkt. Ndumbaro Amesema hayo wakati akizindua rasmi Tamasha la 43 la Sanaa na Utamaduni la Bagamoyo 2024, ambalo kwa mwaka huu linashirikisha nchi zaidi ya 9 duniani huku likitoa fursa za ajira na biashara kwa wananchi wa Bagamoyo na washiriki wa tamasha hilo za moja kwa moja kwa uwepo wake.

“Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Oktoba 23, 2024 lina nchi zaidi ya 9, ikiwemo Ujerumani, Afrika ya Kusini na Zambia, Mayote, India, Brazili, Hispania na Bostwana.


Fursa kwa wakazi wa Bagamoyo ambao wataweza kufanya biashara pamoja na kuonyesha bidhaa zao ili waweze kunufaika kiuchumi.