Faustine Ndugulile amechaguliwa kuwa Mkurugenzi kikanda wa Afrika katika Shirika la Afya Duniani (WHO).
Dk Ndugulile, mtaalam wa afya ya umma ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Jimbo la Kigamboni jijini Dar es Salaam alikuwa mmoja wa wagombea watano waliojitokeza kurithi mikoba ya Dk Matshidiso Moeti.
Dk Moeti, raia wa Botswana anatarajiwa kuhitimisha muhula wake wa pili kama Mkurugenzi wa Kanda wa WHO katika kikao cha 74 kinachoendelea cha Kamati ya Kanda ya Afrika ya WHO huko nchini Congo Brazzaville tangu Agosti 26 hadi Agosti 30, 2024.
Rais Samia Suluhu Hassan alituma pongezi zake za dhati kwa Dk Ndugulile kwa kuchaguliwa akisema, “Umeifanya nchi yetu kuwa na fahari, na bara letu litafaidika sana na kazi yako.”