Na Magrethy Katengu, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Isdor Mpango ameongoza mamia ya watanzani leo Jijini Dar es salaam Viwanja vya Kareemjee katika Maombezo ya kuuga Mwili wa aliyekuwa Waziri Mkuu Mastaafu wa Tanzania Edward Ngoyayi Lowassa
Akitoa Salamu za Taifa amesema Watanzania hawana budi kumshukuru Mungu kwa kila jambo lililotokea kwani alitupatia zawadi ya Edward Lowassa na katika kipindi cha uhai wake alifanya mema mengi aliitumikia Taifa lake kama mzalendo hakuwa mtu wa kuyumbishwa.
Hata hivyo akigusia historia fupi ya maisha yake na yale aliyoayafanya amesema alikuwa mtetezi Wawananchi wa Jimbo la Monduli katika maisha yake alipokuwa Waziri wa Maji Mkuu alifanya jitihada za kusaidia baadhi ya mikoa maji ipate Maji ikiwemo Kahama .
“Kila alipokuwa akisimama alitaja vipaumbele vya Taifa elimu elimu elimu alihakikisha utekelezaji wa sera kila kata pia ujenzi wa Chuo cha UDOM pia alikuwa mwanamazingira alihimiza uhifadhi na utunzaji hivyo mchango wake huo unatukumbusha sanaa watanzania ” amesema Mpango.
Sambamba na hayo Maisha yake ya Kiroho Alikuwa na bidii ya kumwabudu Mungu alikumbusha watu kanisani kuwa Kumcha Mungu ni chanzo cha hekima na maarifa hivyo msiba huo upokelewe kwa imani na Kila Mtanzania.
Aidha Watanzani Msibaa huu utumike kudumisha Upendo na Mshikamano wa Taifa letu kwani Bwana ametoa na sasa ametoa jina lake lihimidiwe Amina
Naye Rais wa Zanzibar Ally Hussan Mwinyi ametoa salam za pole kwa familia amesema amejifunza mengi sana kwa Marehemu Edward Lowasa kwani wakati wa uhai wake alikuwa na Mzalendo na alishirikiana na makundi mbambali kuliletea Taifa Maendeleo.
Naye Mtoto wa Marehemu Waziri Mstaafu Ambaye Pia Mbunge wa Monduli Fredy Edward Lowassa amesema walimuuguza baba yao kwa muda mrefu na Rais Dkt Samia Suluhu Hassani alikuwa karibu sana na familia yao wakati wanamuuguza hivyo hata kabla ya Umauti kumkuta alimuagiza Mkuu wa Majeshi kuwa karibu kupambania uhai wake lakini siku ya februari 10 Mungu aliruhusu alale mauti .
Awali Mchungaji wa Kanisa na KKT Usharika wa Azania Front ,Joseph Mlaki alitoa neno la faraja kwa wafiwa amehubiri kupitia biblia kitabu cha Wakorintho (1)5:16-18 kinachosema
16 Furahini siku zote;
17 ombeni bila kukoma;
18 shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kiristo Yesu
Zaburi 32 ;8
Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.
Aidha Watanzani Msibaa huu utumike kudumisha Upendo na Mshikamano wa Taifa letu kwani Bwana ametoa na sasa ametoa jina lake lihimidiwe Amina