Na Jumanne Magazi, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Diwani wa Kata ya Makulumla Wilaya ya Ubungo, Jijiji Dar es Salaam, Bakari Kimwanga, amesema kumekuwa na taarifa nyingi zinazohusiana na kutekwa kwa watoto wakiwa shuleni ambapo amesema taarifa hizo kuwa sio nyingi si za kweli.

Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara maalum uliofanyika katika shule za msingi za Dk. Omar Ali Juma na Karume uliowakutanisha viongozi wa kiserikai na chama wazazi walimu kamati ya ulinzi na usalama wakiwemo wadau wa elimu kutoka Kata ya Makurumla.

“Wazazi mnatakiwa kuacha kuzua taharuki pindi mnaposikia uzushi unaozagaa kuhusiana na kutekwa au kuuawa kwa watoto pindi wanapokuwa shuleni taarifa hizi si za kweli” amesema.

Kimwanga amesema kuna haja ya wazazi kuwa na ushirikiano baina yao na walimu ili kujua maendeleo kiujumla ya watoto wao kielimu na kiusalama.

Kwa upande wake mwenyekiti wa usalama kata ya Makulumla afande Emanuel amewahakikishia wazazi na walezi kuwa hali ya usalama ya watoto katika kata hiyo ni salama ambapo wamesema Jeshi la Polisi liko makini na linaendelea na upelelezi juu ya kuwepo kwa taarifa hizo za uzushi zilizoibuka hivi karibuni katika baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es Salaam za kupotea au kutekwa kwa watoto wao pindi wawapo shuleni taarifa ambazo zimekanushwa vikali na Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo maalum Kamishina Msaidizi Jumanne Muliro kwa kuziita ni za uzushi zinazolenga kuleta taharuki kwenye jamii.

Kwa upande wake Afisa Elimu wa shule za msingi na awali wa Manispaa ya Ubungo Denis Nyoni amewaomba walimu wa shule zote za kata hiyo kuweka utaratibu wa kutambua watoto wanapofika shuleni ikiwemo kuweka utaratibu wa kuwatambua na kuita majina asubuhi na jioni wakifika shuleni na wanapokaribia Kutoka ili kubaini na kujiridhisha uwepo wa watoto shuleni.

” Wazazi tunapaswa kulinda watoto wetu kwani Jukumu la kulinda watoto wetu ni Jukumu letu wote” amesema.

Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Kimamba Mohamed Mselemi amesema kwa upande wao kama viongozi wa Serikali wameanzisha mpango mkakati ambao unashirikisha wazazi na walimu wakuu wa shule zilizopo kata hiyo ya Makurumla.

Pia ametoa rai kwa wazazi na walezi kuwapa utaratibu wa kuwapa pesa kiasi cha Shilingi mia 500 ili iwasaidie kwa ajili ya chakula jambo litasaidia kuwapa utulivu watoto wawapo shuleni.

Amesema ” wazazi tuna kila sababu ya kufuatilia mienendo ya watoto wetu kwa kila hatua wanapokuwa shuleni badala ya kuwaachia walimu pekee malezi ya watoto wetu jambo ambalo kitaalamu sio sahihi”

Kwa upande wao mmoja wa wazazi wa wanafunzi wanasoma shule za msingi za karume na Dkt.Omar aliyetambulika kwa jina moja la Bi.Hadija amesema wazazi kuacha kuwaendekeza watoto kwa kuwapa muda wa kucheza michezo isiyo na tija pamoja na kuangalia tamthilia jambo linalopelekea kushuka kitaaluma hali inayosababisha mmong’onyoko wa maadili.

Please follow and like us:
Pin Share