MKUU wa Wilaya ya Ubungo, Hassan Bomboko amesema kupitia dira mpya anatamani viongozi kuangalia muelekeo wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kutafsiri maono yake katika misingi ya ujenzi wa taifa lenye usawa, haki na uhuru wa watu.

Bomboko amesema hayo katika kikao cha Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ilipokutana na Bodi ya Ushauri ya Maendeleo ya Ubungo ‘DCC’ kujadili  mafanikio ya Dira ya Taifa mwaka 2000/2025  pamoja na kuchangia juu ya  malengo ya dira mpya.

“Tutatumia falsafa ya R nne katika kuhakikisha yale yote ambayo tunayahitaji katika dira ya taifa ya maendeleo, ikiwemo maridhiano, ustamilivu, mabadiliko na kujenga upya ambapo misingi yake ni utaifa wetu,” amesema Bomboko.

Amewataka kutumia kikao hicho kama nyenzo na daraja la kujenga upya taifa pamoja na jamii ya watu wa Ubungo kwa kujadiliana na kubadili fikra kwa ajili ya kukusanya maoni.

“Nawaomba washiriki wote na nafasi zao, nyie mnapenda taifa lenu Kwa kipindi hicho Cha dira ya mwaka 2025 nyie ndiyo mtakuwa mmeiyamua” alisema.

Please follow and like us:
Pin Share