MLEZI wa Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM ),Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa, amewasihi wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi mkoani humo kujitokeza kwa wingi kutekeleza haki zao za msingi ya kwa kuwachagua viongozi wa Chama hicho.
Amesema kwani hatua hiyo ni ya kidemokrasia katika kufanya maamuzi sahihi ya kuwapigia kura za ndio wagombea wote wanaopeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa zinazotarajia kufanyika ifikapo tarehe 27 Novemba mwaka huu.
Dkt Dimwa hiyo ametoa kauli hiyo leo wakati akiwahutubia maelfu ya wananchi wa Mkoa huo ikiwa ni hatua ya kufungua kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa upande wa Chama hicho huko Wilaya ya Tanganyika Kata ya Ikola, Kijiji cha Mchangani,Kitongoji cha Kajinga Uwanja wa Like Tanganyika ‘A’.
Katika maelezo yake Dkt.Dimwa, amewasisitiza wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kuweka kando tofauti zao za makundi yaliyojitokeza katika uchaguzi wa ndani wa kura za maoni na badala yake wabaki na kundi moja la CCM linalounga mkono wagombea wateule ili Chama hicho kipate shindi wa kishindo katika uchaguzi huo.
Dkt.Dimwa,alisema CCM ina sababu na dhamira ya dhati ya kupata ushindi mkubwa kutokana na Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, kutekeleza kwa ufanisi miradi mbalimbali ya maendeleo inayogharimu kiasi cha zaidi ya shilingi Trioni 1.3 katika Mkoa wa Katavi
Kwa upande wa wananchi akizungumza kwa niaba bi Maryam Maftah amesema jitihada za Serikali kupitia CCM zinaoneka kwani Mhe.Rais Mama Samia Suluh anajitahidi kutuletea Maendeleo katika nchi bila ya ubaguzi hivyo ni vyema wananchi tuunge mkono.