Makamu wa Rais,Kamala Harris ameonekana kuungwa mkono  na wajumbe wa kutosha wa Chama cha Democratic  kuteuliwa kuwa mgombea wa urais wa chama hicho.

Utafiti uliofanywa na Shirika la Habari la Associated Press  umegunduakuwa zaidi ya wajumbe 1,976 wako tayari kupiga kura ya ndio katika Kongamano la Kitaifa la Kidemokrasia (DNC).

Hatahivyo taarifa zinasema kuwa uidhinishaji huo sio rasmi kisheria, lakini ikiwa jumla ya wajumbe watamuunga mkono Harris kuanzia sasa  hadi  siku ya kupiga kura basi kuna uwezekano mkubwa wa kushinda.

Mpaka sasa  wajumbe  kutoka angalau majimbo 27 wamekiri  kumuunga   mkono Kamala Harris  huku  uchaguzi huo ukipangwa kufanyika  Agosti mosi  hadi Agosti 7.

Utafiti huu ni dalili ya msingi wa kumuunga mkono Kamala Harris baada ya Rais Joe Biden kujiondoa katika kinyang’anyiro hicho siku ya Jumapili.

Please follow and like us:
Pin Share