• Washiriki waweka rekodi

WIZARA ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, kwa kushirikiana na SoftVentures, Tume ya TEHAMA (ICTC) na Chama cha Watoa Huduma za Intaneti Tanzania (TISPA), inatangaza kuingia ushirikiano wa kimkakati na Deloitte kwa ajili ya Tuzo za TEHAMA 2025, pamoja na matokeo ya uteuzi wa kazi za washiriki wa tuzo hizo ambayo hayajawahi kushuhudiwa.

Ushirikiano wa Kimkakati na Deloitte
Deloitte inajiunga na Tuzo za TEHAMA ili kuimarisha utawala na uaminifu wa tuzo hizi. Kampuni
hiyo itafanya yafuatayo:
● Kutoa ushauri na usimamizi katika mchakato wa tathmini;
● Kusaidia katika usimamizi wa utawala na hatari; na
● Kuchangia maarifa ya sekta ili kuendeleza mabadiliko ya kidijitali Tanzania.

“Deloitte inajivunia kushirikiana na Tuzo za TEHAMA 2025 katika kutambua na kusherehekea
ubora wa TEHAMA nchini Tanzania,” alisema Suzana Patrick, Mshauri Mwandamizi wa Deloitte
Tanzania. “

Ushirikiano huu unaonesha dhamira yetu ya kukuza uvumbuzi, utawala bora, na
ukuaji endelevu wa kidijitali.”

Akizungumzia ushirikiano huu, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA, Dkt. Nkundwe Mwasaga, alisema:

“Kwa niaba ya kamati ya maandalizi ya Tuzo za TEHAMA, tunaamini kuwa utawala
imara na uwazi ni muhimu katika kutambua ubora halisi katika sekta ya TEHAMA. Ushirikiano na Deloitte kwa Tuzo za TEHAMA 2025 unathibitisha dhamira yetu ya kuhakikisha viwango vya juu
zaidi katika mchakato wa tathmini. Ushirikiano huu unahakikisha kuwa uvumbuzi, athari, na uadilifu vinabaki kuwa msingi wa tuzo hizi tunaposherehekea wale wanaobadilisha mustakabali
wa kidijitali wa Tanzania.”

Idadi Kubwa ya Uteuzi
Tuzo hizo zimepokea uteuzi wa kazi 380 katika vipengele 10, huku kukiwa na ushiriki mkubwa katika vipengele vidogo 21 kati ya 22. Maeneo makuu ya ushindani ni pamoja na:
● Matumizi ya TEHAMA katika Elimu, Fedha, na Afya
● Uvumbuzi wa Usalama wa Mtandao
● Mbinu Bora za Ulinzi wa Taarifa
● Teknolojia Zinazochipukia
● Miradi ya TEHAMA katika Sekta ya Umma na Binafsi
● Tuzo za Muunganisho wa Mtandao (Mtoa Huduma Bora wa Mawasiliano, ISP, na MNO)
● Utofauti katika Teknolojia (Mvumbuzi Mwanamke, Kiongozi wa Teknolojia Mwanamke,
Ubora wa Wanafunzi)

Sherehe za Tuzo zitafanyika Februari 21, 2025 ambapo katika ukumbi Hotel Gran Meliá, Arusha