Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule akikagua Msingi wa Bweni la Shule ya Sekondari Bombo Wialayani hapo ambao umekwama tangu 2017 kutokana na Wananchi kushindw akujitokeza kuchangia ujenzi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule akikagua, akiwa ameongozana na Wataalamu kutoka Wilayani kukagua Madarasa yaliyojengwa tangu 2017 bila kukamilika.
Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Sinyamule ameagiza wa Kata ya Bombo awekwe ndani chini ya ulinzi mkali kwa saa 8 kutokana na kushindwa kusimamia ujenzi wa bweni la shule ya Sekondari Bombo na kumtaka apewa siku 2 kuleta maelezo kwa nini asichukuliwe hatua.
Dc Sinyamule, amefikia uamuzi huo mara baada ya wataalamu wa kutaka hela za kujenga bweni la Shule ya sekondari ya Bombo zihamishiwe shule nyingine kutokana na wananachi wa kata ya Bombo kutotoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha ujenzi wa bweni hilo unakamilka.
“Fedha za serikali ( P4R) zilipelekwa tangu mapema 2017 na mradi ulitakiwa kuisha Nov. 2017 na Ikitegemewa kuwa kuanzia hapo ujenzi wa bweni uanze na mpaka leo nimefika hapa March 2018 bado hata msingi haujakamilika kujengwa na kutoa sababu zisizo na tija.
Mtendaji huyu ameshindw akusimamia Vizuri majukumu yake ya kuhamasisha watu kushiriki katika miradi ya maendeleo hasa ujenzi wa bweni la shule hii ambayo serikali ilishatoa fedha kilichotakiwa ni nguvu ya wananchi.
Amesema kuwa Wananchi wa eneo la Bombo hawajitokezi kwenye kusaidia kazi. na Mtendaji kama muhamasishaji hajitumi, hivyo nimeamuru awekwe chini ya ulinzi masaa 8 kwani hela za Serikali zakaa bila kazi kwa muda mrefu. Zaichafulia jina Wilaya yangu , Kwani tunaonekana wote ni wazembe.
Dc Sinyamule amesema ni heri tushauri hela hizi zihamishiwe mahali ambako wananchi wako tayari kupokea maendeleo na kushiriki; kwani wanaohitaji fedha hizi ni wengi kwani Viongozi wa kisiasa hawatoi ushirikiano, na wanachangia kufanya kazi ichelewe.
Amesema Serikali ya CCM ina dhamira njema na haina ubaguzi katika maendeleo. lakini wanaoletewa maendeleo wanaleta uzembe; nitamshauri Waziri hela hizi zipelekwe kumalizia shule ambazo wananchi wameshajitolea zinangoja umaliziaji.
DC Sinyamule ametaja kuwa shule hiyo ililetewa Tshs Milioni 245 kwa ajili ya kujenga madarasa 4, choo na mabweni 2. Ambapo tangu Aug. 2017 kazi ya ujenzi wa madarasa ilikuwa imekamilika. Lakini baada ya hapo hakuna kilichofanyika kwa miezi 7 sasa huu sio utendaji kazi wa serikali ya awamu ya tano.