Na Mussa Augustine, Jamhuri
Kampuni ya Dahua Teknoloji inayojihusisha na uuzaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo vifaa vya ulinzi imesema serikali ya awamu ya sita imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuweka Mazingira rafiki kwa Wawekezaji hali ambayo imechochea Wawekezaji Wengi kuja kuwekeza nchini Tanzania.
Akizungumza na Jamhuri Meneja bidhaa wa Kampuni hiyo Samsoni Ibrahim alisema kuwepo kwa hali ya amani na utulivu nchini imechangia kwa kiasi kikubwa wafanyabishara kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo china kuja kuwekeza katika sekta mbalimbali nakukuza uchumi wa Tanzania.
” Napenda kushukuru Serikali ya Tanzania na rais wetu Mama Samia kwa Kutuongozea nchi yetu kwa kutuwekea mazingira ya amani na hata wawekezaji hao wanaokuja wanakuta mazingira ya ko vizuri hivyo inatupeleka hata sisi kupata fursa ya kufanya kazi na nchi mbalimbali,hivyo ni jambo zuri sana linafanywa na serikali ya awamu ya sita,alisema Ibrahim.
Aidha aliongeza kuwa Kampuni ya Dahua Teknologe yenye makao yake makuu nchini china inazalisha vifaa vya kusimamia usalama wa watu na mali zao kama vile magari,pamoja na kudhibiti vitendo vya uhalifu kwani uhalifu mwingi unafanyika kwa kutumia usafiri wa magari na pikipiki.
“Vifaa tulivyo navyo siyo kwa ajili ya kudhibiti usalama wa watu na mali zao pakee lakini pia tuna vifaa aina nyingi ikiwemo vifaa vya kufuatilia data muhimu kwa serikali,kampuni binafsi hata Benki wanapotaka kupata data mbalimbali za kibiashara,tunateknolojia za kisasa aina zote zinazofaa kwenye ulinzi lakini pia usalama wa biashara( Business Intelligence) alisema.
Nakuongeza kuwa” pia tuna vifaa vya kuwezesha kufanya mikutano kwa njia ya mitandao ( Video Conference) pamoja na vifaa aina ya Droni zinazotumika kurekodi picha za matukio angani,hivyo ameziomba taasisi mbalimbali kutembelea sehemu yao ya kuuzia bidhaa zao Da salaam.